Isaiah 66:3 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Lakini watu hawa wanafanya wanavyotaka: Wananitolea tambiko ya ng'ombe na mara wanaua watu kutambikia. Wananitolea sadaka ya mwanakondoo na pia wanamvunja mbwa shingo. Wananitolea tambiko ya nafaka na pia kupeleka damu ya nguruwe. Wanachoma ubani mbele yangu na kwenda kuabudu miungu ya uongo. Hao wamechagua kufuata njia zao wenyewe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini yeyote atoaye dhabihu ya fahali ni kama yeye auaye mtu, na yeyote atoaye sadaka ya mwana-kondoo, ni kama yule avunjaye shingo ya mbwa. Yeyote atoaye sadaka ya nafaka, ni kama yule aletaye damu ya nguruwe, na yeyote afukizaye uvumba wa kumbukumbu, ni kama yule aabuduye sanamu. Wamejichagulia njia zao wenyewe, nazo nafsi zao zinafurahia machukizo yao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yeye achinjaye ng'ombe ni kama yeye amwuaye mtu; na yeye atoaye dhabihu ya mwana-kondoo ni kama yeye avunjaye shingo ya mbwa; na yeye atoaye matoleo ni kama yeye atoaye damu ya nguruwe; na yeye afukizaye uvumba ni kama yeye abarikiye sanamu; naam, wamezichagua njia zao wenyewe, na nafsi zao zafurahia machukizo yao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Lakini watu hawa wanafanya wanavyotaka: wananitolea tambiko ya ng'ombe na mara wanaua watu kutambikia. Wananitolea sadaka ya mwanakondoo na pia wanamvunja mbwa shingo. Wananitolea tambiko ya nafaka na pia kupeleka damu ya nguruwe. Wanachoma ubani mbele yangu na kwenda kuabudu miungu ya uongo. Hao wamechagua kufuata njia zao wenyewe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini ye yote atoaye dhabihu ya fahali ni kama yeye auaye mtu, na ye yote atoaye sadaka ya mwana-kondoo, ni kama yule avunjaye shingo ya mbwa; ye yote atoaye sadaka ya nafaka, ni kama yule aletaye damu ya nguruwe, na ye yote afukizaye uvumba wa kumbukumbu, ni kama yule aabuduye sanamu. Wamejichagulia njia zao wenyewe, nazo nafsi zao zinafurahia machukizo yao,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini yeyote atoaye dhabihu ya fahali ni kama yeye auaye mtu, na yeyote atoaye sadaka ya mwana-kondoo, ni kama yule avunjaye shingo ya mbwa. Yeyote atoaye sadaka ya nafaka, ni kama yule aletaye damu ya nguruwe, na yeyote afukizaye uvumba wa kumbukumbu, ni kama yule aabuduye sanamu. Wamejichagulia njia zao wenyewe, nazo nafsi zao zinafurahia machukizo yao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yeye achinjaye ng'ombe ni kama yeye amwuaye mtu; na yeye atoaye dhabihu ya mwana-kondoo ni kama yeye avunjaye shingo ya mbwa; na yeye atoaye matoleo ni kama yeye atoaye damu ya nguruwe; na yeye afukizaye uvumba ni kama yeye abarikiye sanamu; naam, wamezichagua njia zao wenyewe, na nafsi zao zafurahia machukizo yao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Lakini watu hawa wanafanya wanavyotaka: Wananitolea tambiko ya ng'ombe na mara wanaua watu kutambikia. Wananitolea sadaka ya mwanakondoo na pia wanamvunja mbwa shingo. Wananitolea tambiko ya nafaka na pia kupeleka damu ya nguruwe. Wanachoma ubani mbele yangu na kwenda kuabudu miungu ya uongo. Hao wamechagua kufuata njia zao wenyewe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Achinjaye ng'ombe huwa kama mwenye kuua mtu, naye atoaye kondoo kuwa ng'ombe ya tambiko huwa kama mwenye kunyonga mbwa, naye atoaye vyakula kuwa vipaji vya tambiko humwaga nazo damu za nguruwe, avukizaye uvumba hutambikia mizimu: hao ndio waliojichagulia njia zao, nazo roho zao zikapendezwa na matapisho yao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yeye achinjaye ng’ombe ni kama yeye amwuaye mtu; na yeye atoaye dhabihu ya mwana-kondoo ni kama yeye avunjaye shingo ya mbwa; na yeye atoaye matoleo ni kama yeye atoaye damu ya nguruwe; na yeye afukizaye uvumba ni kama yeye abarikiye sanamu; naam, wamezichagua njia zao wenyewe, na nafsi zao zafurahia machukizo yao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini watu hawa wanafanya wanavyotaka: wananitolea sadaka ya ngombe na tena wanaua watu kwa kutambikia. Wananitolea sadaka ya mwana-kondoo na vilevile wanaua imbwa. Wananitolea sadaka ya unga na vilevile wanatolea damu ya nguruwe. Wanachoma ubani mbele yangu na kwenda kuabudu miungu ya uongo. Hao wamechagua kufuata njia zao wenyewe.