Isaiah 66:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sikilizeni neno la Mwenyezi-Mungu, enyi msikiao neno lake mkatetemeka: “Ndugu zenu ambao wanawachukia, na kuwapiga marufuku kwa sababu yangu, wamesema kwa dharau ‘Mungu na aoneshe utukufu wake, nasi tuwaone nyinyi mkishinda!’ Lakini wao wenyewe ndio watakaoaibishwa!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sikieni neno la Mwenyezi Mungu, ninyi mtetemekao kwa neno lake: “Ndugu zenu wanaowachukia ninyi na kuwatenga ninyi kwa sababu ya Jina langu, wamesema, ‘Mwenyezi Mungu na atukuzwe, ili tupate kuona furaha yenu!’ Hata sasa wataaibika.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lisikilizeni neno la Bwana, ninyi mtetemekao kwa sababu ya neno lake; Ndugu zenu wawachukiao ninyi, waliowatupa kwa ajili ya jina langu, wamesema, Na atukuzwe Bwana, tupate kuiona furaha yenu; lakini watatahayarika.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sikilizeni neno la Mwenyezi-Mungu, enyi msikiao neno lake mkatetemeka: “Ndugu zenu ambao wanawachukia, na kuwapiga marufuku kwa sababu yangu, wamesema kwa dharau: ‘Mungu na aoneshe utukufu wake, nasi tuwaone nyinyi mkishinda!’ Lakini wao wenyewe ndio watakaoaibishwa!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sikieni neno la BWANA, ninyi mtetemekao kwa neno lake, “Ndugu zenu wanaowachukia ninyi na kuwatenga ninyi kwa sababu ya Jina langu, wamesema, ‘BWANA na atukuzwe, ili tupate kuona furaha yenu!’ Hata sasa wataaibika.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sikieni neno la bwana, ninyi mtetemekao kwa neno lake: “Ndugu zenu wanaowachukia ninyi na kuwatenga ninyi kwa sababu ya Jina langu, wamesema, ‘ bwana na atukuzwe, ili tupate kuona furaha yenu!’ Hata sasa wataaibika.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lisikilizeni neno la BWANA, ninyi mtetemekao kwa sababu ya neno lake; Ndugu zenu wawachukiao ninyi, waliowatupa kwa ajili ya jina langu, wamesema, Na atukuzwe BWANA, tupate kuiona furaha yenu; lakini watatahayarika.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sikilizeni neno la Mwenyezi-Mungu, enyi msikiao neno lake mkatetemeka: “Ndugu zenu ambao wanawachukia, na kuwapiga marufuku kwa sababu yangu, wamesema kwa dharau ‘Mungu na aoneshe utukufu wake, nasi tuwaone nyinyi mkishinda!’ Lakini wao wenyewe ndio watakaoaibishwa!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lisikilizeni Neno la Bwana, mtetemekao mkilisikia Neno la Bwana! Ndugu zenu wanaowachukia ninyi, waliowafukuza kwa ajili ya Jina langu walisema: Bwana na autokeze utukufu wake, tuone, mkiufurahia! Lakini wao watapatwa na soni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lisikilizeni neno la BWANA, ninyi mtetemekao kwa sababu ya neno lake; Ndugu zenu wawachukiao ninyi, waliowatupa kwa ajili ya jina langu, wamesema, Na atukuzwe BWANA, tupate kuiona furaha yenu; lakini watatahayarika.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Musikilize neno la Yawe, enyi munaotetemeka kwa sababu ya neno lake. Wandugu zenu ambao wanawachukia, na kuwafukuza kwa sababu yangu, wamesema hivi kwa kuwachekelea: Mungu aonyeshe utukufu wake, nasi tuwaone ninyi mukishinda! Lakini wao wenyewe ndio watakaopata haya!