Isaiah 66:8 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ni nani aliyepata kusikia jambo kama hilo? Ni nani aliyewahi kuona jambo kama hilo? Je, nchi nzima yaweza kuzaliwa siku moja? Je, taifa zima laweza kuzaliwa mara moja? Maana Siyoni, mara tu alipoanza kuona uchungu, alijifungua watoto wake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ni nani amepata kusikia jambo kama hili? Ni nani amepata kuona mambo kama haya? Je, nchi yaweza kuzaliwa kwa siku moja, au taifa laweza kutokea mara moja? Mara Sayuni alipoona uchungu, alizaa watoto wake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ni nani aliyesikia neno kama hili? Ni nani aliyeona mambo kama haya? Je! Nchi yaweza kuzaliwa siku moja? Taifa laweza kuzaliwa mara? Maana Sayuni, mara alipoona utungu, Alizaa watoto wake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ni nani aliyepata kusikia jambo kama hilo? Ni nani aliyewahi kuona jambo kama hilo? Je, nchi nzima yaweza kuzaliwa siku moja? Je, taifa zima laweza kuzaliwa mara moja? Maana Siyoni, mara tu alipoanza kuona uchungu, alijifungua watoto wake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ni nani amepata kusikia jambo kama hili? Ni nani amepata kuona mambo kama haya? Je, nchi yaweza kuzaliwa kwa siku moja au taifa laweza kutokea mara? Mara Sayuni alipoona utungu, alizaa watoto wake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ni nani amepata kusikia jambo kama hili? Ni nani amepata kuona mambo kama haya? Je, nchi yaweza kuzaliwa kwa siku moja, au taifa laweza kutokea mara? Mara Sayuni alipoona utungu, alizaa watoto wake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ni nani aliyesikia neno kama hili? Ni nani aliyeona mambo kama haya? Je! Nchi yaweza kuzaliwa kwa siku moja? Taifa laweza kuzaliwa mara? Maana Sayuni, mara alipopata uchungu, Alizaa watoto wake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ni nani aliyepata kusikia jambo kama hilo? Ni nani aliyewahi kuona jambo kama hilo? Je, nchi nzima yaweza kuzaliwa siku moja? Je, taifa zima laweza kuzaliwa mara moja? Maana Siyoni, mara tu alipoanza kuona uchungu, alijifungua watoto wake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yuko nani aliyesikia kama hayo? Yuko nani aliyeona kama hayo? Inakuwaje, nchi ikitokezwa siku moja? Inakuwaje, ukoo mzima wa watu ukizaliwa kwa mara moja? Kwani Sioni uliposhikwa na uchungu papo hapo umewazaa watoto wake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ni nani aliyesikia neno kama hili? Ni nani aliyeona mambo kama haya? Je! Nchi yaweza kuzaliwa siku moja? Taifa laweza kuzaliwa mara? Maana Sayuni, mara alipoona utungu, Alizaa watoto wake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ni nani aliyepata kusikia jambo kama lile? Ni nani aliyepata kuona jambo kama lile? Inchi nzima inaweza kuzaliwa kwa siku moja? Taifa zima linaweza kuzaliwa kwa mara moja? Maana mara moja tu Sayuni ulipoanza kupata uchungu, palepale ukazaa watoto wake.