Isaiah 66:9 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Je, nitawatunza watu wangu mpaka karibu wazaliwe, halafu niwazuie wasizaliwe? Au mimi mwenye kuwajalia watoto, nitafunga kizazi chao? Mimi Mungu wenu nimesema.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Je, nilete mwana hadi wakati wa kuzaliwa na nisizalishe?” asema Mwenyezi Mungu. “Je, nifunge tumbo la uzazi wakati mimi ndiye nizalishaye?” asema Mungu wako.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Je! Mimi nilete wana karibu na kuzaliwa, nisizalishe? Asema Bwana; mimi nizalishaye, je! Nilifunge tumbo? Asema Mungu wako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Je, nitawatunza watu wangu mpaka karibu wazaliwe, halafu niwazuie wasizaliwe? Au mimi mwenye kuwajalia watoto, nitafunga kizazi chao? Mimi Mungu wenu nimesema.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Je, nilete hadi wakati wa kuzaliwa na nisizalishe?” asema BWANA. “Je, nifunge tumbo la uzazi wakati mimi ndiye nizalishaye?” asema Mungu wako.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Je, nilete mwana hadi wakati wa kuzaliwa na nisizalishe?” asema bwana. “Je, nifunge tumbo la uzazi wakati mimi ndiye nizalishaye?” asema Mungu wako.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Je! Mimi nilete wana karibu na kuzaliwa, nisizalishe? Asema BWANA; mimi nizalishaye, je! Nilifunge tumbo? Asema Mungu wako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Je, nitawatunza watu wangu mpaka karibu wazaliwe, halafu niwazuie wasizaliwe? Au mimi mwenye kuwajalia watoto, nitafunga kizazi chao? Mimi Mungu wenu nimesema.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Je? Mimi nifikishe watoto pa kuzaliwa, nisiwazalishe? ndivyo, Bwana anavyosema. Je? Mimi ninapozalisha, nilifunge tumbo la mama? ndivyo, Mungu wako anavyosema.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Je! Mimi nilete wana karibu na kuzaliwa, nisizalishe? Asema BWANA; mimi nizalishaye, je! Nilifunge tumbo? Asema Mungu wako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Namna gani ninaweza kumufikisha mutoto kwa saa ya kuzaliwa, halafu nimuzuize asizaliwe? –Ni Yawe anayesema hivyo.– Au mimi mwenye kuwajalia watoto, namna gani nitafunga uzazi? –Ni Mungu wenu anayesema hivyo.