Isaiah 7:17 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu atakuletea wewe pamoja na watu wako na jamii yote ya kifalme siku za taabu kuliko zile zote zilizowahi kutokea tangu wakati watu wa Efraimu walipojitenga na Yuda; yaani, atawaleteeni mfalme wa Ashuru.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwenyezi Mungu ataleta juu yako pamoja na watu wako na juu ya nyumba ya baba yako, nyakati ambazo hazijawahi kuwako tangu Efraimu alipojitenga na Yuda: naye Mwenyezi Mungu atawaleteeni mfalme wa Ashuru.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana ataleta juu yako, na juu ya watu wako, na juu ya nyumba ya baba yako, siku zisizokuja bado, tangu siku ile aliyoondoka Efraimu kutoka katika Yuda; yaani, mfalme wa Ashuru.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu atakuletea wewe pamoja na watu wako na jamii yote ya kifalme siku za taabu kuliko zile zote zilizowahi kutokea tangu wakati watu wa Efraimu walipojitenga na Yuda; yaani, atawaleteeni mfalme wa Ashuru.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
BWANA ataleta juu yako, juu ya watu wako na juu ya nyumba ya baba yako wakati ambao haujawahi kuwako tangu Efraimu alipojitenga na Yuda, atawaleteeni mfalme wa Ashuru.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
bwana ataleta juu yako, juu ya watu wako, na juu ya nyumba ya baba yako wakati ambao haujawahi kuwako tangu Efraimu alipojitenga na Yuda: yeye atawaleteeni mfalme wa Ashuru.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA ataleta juu yako, na juu ya watu wako, na juu ya nyumba ya baba yako, siku zisizokuja bado, tangu siku ile aliyoondoka Efraimu kutoka katika Yuda; yaani, mfalme wa Ashuru.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu atakuletea wewe pamoja na watu wako na jamii yote ya kifalme siku za taabu kuliko zile zote zilizowahi kutokea tangu wakati watu wa Efraimu walipojitenga na Yuda; yaani, atawaleteeni mfalme wa Ashuru.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Bwana atawaletea ninyi, wewe nao wa ukoo wako nao wa mlango wa baba yako, siku zisizokuja bado kuanzia siku ile, Waefuraimu walipojitenga kwao Wayuda; itakuwa hapo, mfalme wa Asuri atakapokuja.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA ataleta juu yako, na juu ya watu wako, na juu ya nyumba ya baba yako, siku zisizokuja bado, tangu siku ile aliyoondoka Efraimu kutoka katika Yuda; yaani, mfalme wa Ashuru.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe atakuletea wewe pamoja na watu wako na jamaa yote ya kifalme siku za taabu kuliko zile zote zilizotokea tangu wakati watu wa Efuraimu walipojitenga na watu wa Yuda; ni kusema, atawaletea ninyi mufalme wa Asuria.