Isaiah 7:18 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati huo, Mwenyezi-Mungu atawapigia mruzi watu wa Misri waje kama nzi toka vijito vya mto Nili; na watu wa Ashuru waje kama nyuki kutoka nchi yao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Katika siku ile Mwenyezi Mungu atawapigia filimbi inzi kutoka vijito vya mbali vya Misri, na nyuki kutoka nchi ya Ashuru.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena itakuwa katika siku hiyo Bwana atampigia kelele inzi aliye katika pande za mwisho za mito ya Misri, na nyuki aliye katika nchi ya Ashuru
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati huo, Mwenyezi-Mungu atawapigia mruzi watu wa Misri waje kama nzi toka vijito vya mto Nili; na watu wa Ashuru waje kama nyuki kutoka nchi yao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika siku ile BWANA atawapigia filimbi mainzi kutoka kwenye vijito vya mbali vya Misri na nyuki kutoka nchi ya Ashuru.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika siku ile bwana atawapigia filimbi mainzi kutoka vijito vya mbali vya Misri, na nyuki kutoka nchi ya Ashuru.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena itakuwa katika siku hiyo BWANA atampigia kelele inzi aliye katika pande za mwisho za mito ya Misri, na nyuki aliye katika nchi ya Ashuru
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati huo, Mwenyezi-Mungu atawapigia mruzi watu wa Misri waje kama nzi toka vijito vya mto Nili; na watu wa Ashuru waje kama nyuki kutoka nchi yao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku ile mbung'o walioko mwishoni kwenye mito ya Misri nao nyuki walioko katika nchi ya Asuri Bwana atawapigia miluzi, waje.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena itakuwa katika siku hiyo BWANA atampigia kelele inzi aliye katika pande za mwisho za mito ya Misri, na nyuki aliye katika nchi ya Ashuru
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati huo, Yawe atawapigia muunzi watu wa Misri wakuje kama mainzi toka vijito vya mito Nili; na watu wa Asuria wakuje kama nyuki kutoka inchi yao.