Isaiah 7:20 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati huo, Bwana atakopa wembe kutoka ngambo ya mto Eufrate, yaani mfalme wa Ashuru. Atawanyoa vichwa vyenu, miili yenu na kukatilia mbali pia ndevu zenu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Katika siku ile Bwana atatumia wembe ulioajiriwa kutoka ng’ambo ya Mto, yaani mfalme wa Ashuru, kunyoa nywele za kichwa chako na malaika ya miguu yako, na kuziondoa ndevu zako pia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Katika siku hiyo Bwana atanyoa kichwa na malaika ya miguuni, kwa wembe ulioajiriwa pande za ng'ambo ya Mto, yaani, kwa mfalme wa Ashuru, nao utazimaliza ndevu nazo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati huo, Bwana atakopa wembe kutoka ng'ambo ya mto Eufrate, yaani mfalme wa Ashuru. Atawanyoa vichwa vyenu, miili yenu na kukatilia mbali pia ndevu zenu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika siku ile Bwana atatumia wembe ulioajiriwa kutoka ng'ambo ya Mto yaani mfalme wa Ashuru, kunyoa nywele za kichwa chako, malaika ya miguu yako na kuziondoa ndevu zako pia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika siku ile Bwana atatumia wembe ulioajiriwa kutoka ng’ambo ya Mto, yaani mfalme wa Ashuru, kunyoa nywele za kichwa chako na malaika ya miguu yako, na kuziondoa ndevu zako pia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Katika siku hiyo Bwana atanyoa kichwa na malaika ya miguuni, kwa wembe ulioajiriwa pande za ng'ambo ya Mto, yaani, kwa mfalme wa Ashuru, nao utaziondoa ndevu pia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati huo, Bwana atakopa wembe kutoka ngambo ya mto Eufrate, yaani mfalme wa Ashuru. Atawanyoa vichwa vyenu, miili yenu na kukatilia mbali pia ndevu zenu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku ile Bwana atamtumia mfalme wa Asuri kuwa kama wembe uliokopwa ng'ambo ya lile jito kubwa, awanyoe nywele za vichwa na za miguu, hata za ndevu zitamalizwa zote pia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Katika siku hiyo Bwana atanyoa kichwa na malaika ya miguuni, kwa wembe ulioajiriwa pande za ng’ambo ya Mto, yaani, kwa mfalme wa Ashuru, nao utazimaliza ndevu nazo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati ule, Bwana atalipa wembe kutoka ngambo ya muto Furati, ni kusema mufalme wa Asuria. Atawanyoa vichwa vyenu, miili yenu na ndevu zenu vilevile.