Isaiah 7:8 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwani mji mkuu wa Aramu ni Damasko, na huyo Resini ni mkuu wa Damasko tu. Mji mkuu wa Efraimu ni Samaria, na mwana wa Remalia ni mkuu wa Samaria tu. Mnamo miaka sitini na mitano utawala wa Efraimu utavunjwa; Efraimu halitakuwa taifa tena. Kama hutaamini hutaimarika.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
kwa kuwa kichwa cha Aramu ni Dameski, na kichwa cha Dameski ni Resini peke yake. Katika muda wa miaka sitini na tano, Efraimu atakuwa ameharibiwa kiasi kwamba hataweza tena kuwa taifa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana kichwa cha Shamu ni Dameski, na kichwa cha Dameski ni Resini; na katika muda wa miaka sitini na mitano Efraimu atavunjika vipande vipande, asiwe kabila ya watu tena;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwani mji mkuu wa Aramu ni Damasko, na huyo Resini ni mkuu wa Damasko tu. Mji mkuu wa Efraimu ni Samaria, na mwana wa Remalia ni mkuu wa Samaria tu. Mnamo miaka sitini na mitano utawala wa Efraimu utavunjwa; Efraimu halitakuwa taifa tena. Kama hutaamini hutaimarika.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
kwa kuwa kichwa cha Aramu ni Dameski, na kichwa cha Dameski ni Resini peke yake. Katika muda wa miaka sitini na mitano Efraimu atakuwa ameharibiwa kiasi kwamba hataweza tena kuwa taifa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
kwa kuwa kichwa cha Aramu ni Dameski, na kichwa cha Dameski ni Resini peke yake. Katika muda wa miaka sitini na mitano, Efraimu atakuwa ameharibiwa kiasi kwamba hataweza tena kuwa taifa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana kichwa cha Shamu ni Dameski, na kichwa cha Dameski ni Resini; na katika muda wa miaka sitini na mitano Efraimu atavunjika vipande vipande, asiwe kabila la watu tena;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwani mji mkuu wa Aramu ni Damasko, na huyo Resini ni mkuu wa Damasko tu. Mji mkuu wa Efraimu ni Samaria, na mwana wa Remalia ni mkuu wa Samaria tu. Mnamo miaka sitini na mitano utawala wa Efraimu utavunjwa; Efraimu halitakuwa taifa tena. Kama hutaamini hutaimarika.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani kichwa cha Ushami ni Damasko, nacho kichwa cha Damasko ni Resini, tena miaka 65 itakapopita, Efuraimu atakuwa amepondwa kabisa, wasiwe ukoo tena.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana kichwa cha Shamu ni Dameski, na kichwa cha Dameski ni Resini; na katika muda wa miaka sitini na mitano Efraimu atavunjika vipande vipande, asiwe kabila ya watu tena;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Maana muji mukubwa wa Aramu ni Damasiki, na huyo Resini ni mukubwa wa Damasiki tu. Muji mukubwa wa Efuraimu ni Samaria, na mwana wa Remalia ni mukubwa wa Samaria tu. Katika miaka makumi sita na mitano utawala wa Efuraimu utavunjwa; Efuraimu halitakuwa taifa tena. Kama hautaamini, hautaimarika.