Isaiah 8:14 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mimi nitakuwa kimbilio, nitakuwa pia kama jiwe la kujikwaa, mwamba wa kuziangusha falme za Israeli na Yuda; nitakuwa mtego wa kuwatega na kuwanasa wakazi wa Yerusalemu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
naye atakuwa mahali patakatifu; lakini kwa nyumba zote mbili za Israeli atakuwa jiwe lile linalosababisha watu kujikwaa na mwamba wa kuwaangusha. Kwa watu wa Yerusalemu, atakuwa mtego na tanzi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye atakuwa ni mahali patakatifu; bali ni jiwe la kujikwaza na mwamba wa kujikwaa kwa nyumba za Israeli zote mbili, na mtego na tanzi kwa wenyeji wa Yerusalemu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mimi nitakuwa kimbilio, nitakuwa pia kama jiwe la kujikwaa, mwamba wa kuziangusha falme za Israeli na Yuda; nitakuwa mtego wa kuwatega na kuwanasa wakazi wa Yerusalemu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
naye atakuwa mahali patakatifu; lakini kwa nyumba zote mbili za Israeli atakuwa jiwe lile linalosababisha watu kujikwaa na mwamba wa kuwaangusha. Kwa watu wa Yerusalemu atakuwa mtego na tanzi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
naye atakuwa mahali patakatifu; lakini kwa nyumba zote mbili za Israeli atakuwa jiwe lile linalosababisha watu kujikwaa na mwamba wa kuwaangusha. Kwa watu wa Yerusalemu, atakuwa mtego na tanzi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye atakuwa ni mahali patakatifu; bali ni jiwe la kujikwaza na mwamba wa kujikwaa kwa nyumba za Israeli zote mbili, na mtego na tanzi kwa wenyeji wa Yerusalemu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mimi nitakuwa kimbilio, nitakuwa pia kama jiwe la kujikwaa, mwamba wa kuziangusha falme za Israeli na Yuda; nitakuwa mtego wa kuwatega na kuwanasa wakazi wa Yerusalemu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivyo atakuwa mwenye kutakasa, tena atakuwa jiwe la kujigongea na mwamba wa kujikwalia kwao milango yote miwili ya Isiraeli; nao wakaao Yerusalemu atawawia kama mtego wa tanzi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye atakuwa ni mahali patakatifu; bali ni jiwe la kujikwaza na mwamba wa kujikwaa kwa nyumba za Israeli zote mbili, na mtego na tanzi kwa wenyeji wa Yerusalemu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mimi nitakuwa kimbilio. Nitakuwa vilevile kama jiwe la kujikwaa, jiwe kubwa la kuziangusha falme za Israeli na Yuda. Nitakuwa mutego wa kuwatega na kuwanasa wakaaji wa Yerusalema.