Isaiah 8:19 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baadhi watawaambieni: “Nendeni mkatake shauri kwa mizimu na mizuka iliayo kama ndege; kwani ni kawaida watu kutaka shauri kwa miungu yao, na kutaka shauri kwa wafu kwa ajili ya walio hai.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Watu wanapowaambia ninyi kutafuta ushauri kwa waaguzi na wenye kuongea na mizimu, ambao hunong’ona na kunung’unika, je, watu wasingeuliza kwa Mungu wao? Kwa nini watake shauri kwa wafu kwa ajili ya walio hai?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na wakati watakapokuambia, Tafuta habari kwa watu wenye pepo na kwa wachawi; waliao kama ndege na kunong'ona; je! Haiwapasi watu kutafuta habari kwa Mungu wao? Je! Waende kwa watu waliokufa kwa ajili ya watu walio hai?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baadhi watawaambieni: “Nendeni mkatake shauri kwa mizimu na mizuka iliayo kama ndege; kwani ni kawaida watu kutaka shauri kwa miungu yao, na kutaka shauri kwa wafu kwa ajili ya walio hai.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati watu wanapowaambia ninyi kutafuta ushauri kwa waaguzi na wenye kuongea na mizimu, ambao hunong'ona na kunung'unika, je, watu wasingeuliza kwa Mungu wao? Kwa nini watake shauri kwa wafu kwa ajili ya walio hai?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati watu wanapowaambia ninyi kutafuta ushauri kwa waaguzi na wenye kuongea na mizimu, ambao hunong’ona na kunung’unika, je, watu wasingeuliza kwa Mungu wao? Kwa nini watake shauri kwa wafu kwa ajili ya walio hai?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na wakati watakapokuambia, Tafuta habari kwa watu wenye pepo na kwa wachawi; waliao kama ndege na kunong'ona; je! Haiwapasi watu kutafuta habari kwa Mungu wao? Je! Waende kwa watu waliokufa kwa ajili ya watu walio hai?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baadhi watawaambieni: “Nendeni mkatake shauri kwa mizimu na mizuka iliayo kama ndege; kwani ni kawaida watu kutaka shauri kwa miungu yao, na kutaka shauri kwa wafu kwa ajili ya walio hai.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kama wanawaambia: Watafuteni wajuao kukweza mizimu nao wapunga pepo wanaonong'ona na kusema na sauti ndogo! wajibuni: Wasimtafute Mungu wao, wamwulize? Waulizeje wafu kwa ajili yao walio hai?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na wakati watakapokuambia, Tafuta habari kwa watu wenye pepo na kwa wachawi; waliao kama ndege na kunong’ona; je! Haiwapasi watu kutafuta habari kwa Mungu wao? Je! Waende kwa watu waliokufa kwa ajili ya watu walio hai?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu wamoja watawaambia ninyi: Muombe shauri kwa mizimu na waaguzi wanaolia kama ndege; kwa sababu ni kawaida watu kuomba shauri kwa miungu yao, na kuomba shauri kwa wafu kwa ajili ya wanaokuwa wazima.