Isaiah 8:21 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu watatangatanga nchini wamefadhaika sana na wenye njaa. Na wakiwa na njaa, hasira zitawawaka na kumlaani mfalme wao kadhalika na Mungu wao. Watatazama juu mbinguni
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Watazunguka katika nchi yote, wakiwa na dhiki na njaa. Watakapotaabika kwa njaa, watapatwa na hasira kali, nao, wakiwa wanatazama juu, watamlaani mfalme wao na Mungu wao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao watapita katikati yake, wamedhikika sana na kuwa na njaa; na itakuwa watakapoona njaa, watalalamika na kuapa kwa mfalme wao, na kwa Mungu wao, na kuelekeza nyuso zao juu;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu watatangatanga nchini wamefadhaika sana na wenye njaa. Na wakiwa na njaa, hasira zitawawaka na kumlaani mfalme wao kadhalika na Mungu wao. Watatazama juu mbinguni
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakiwa na dhiki na njaa, watazunguka katika nchi yote, watakapotaabika kwa njaa, watapatwa na hasira kali, wakiwa wanatazama juu, watamlaani mfalme wao na Mungu wao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watazunguka katika nchi yote, wakiwa na dhiki na njaa. Watakapotaabika kwa njaa, watapatwa na hasira kali, nao, wakiwa wanatazama juu, watamlaani mfalme wao na Mungu wao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao watapita katikati yake, wamedhikika sana na kuwa na njaa; na itakuwa watakapoona njaa, watalalamika na kuapa kwa mfalme wao, na kwa Mungu wao, na kuelekeza nyuso zao juu;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu watatangatanga nchini wamefadhaika sana na wenye njaa. Na wakiwa na njaa, hasira zitawawaka na kumlaani mfalme wao kadhalika na Mungu wao. Watatazama juu mbinguni
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hutangatanga katika nchi kwa kuumizwa na ukiwa na njaa; tena kwa kuumizwa na njaa huchafuka, amtukane mfalme wao na mungu wao na kutazama juu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao watapita katikati yake, wamedhikika sana na kuwa na njaa; na itakuwa watakapoona njaa, watalalamika na kuapa kwa mfalme wao, na kwa Mungu wao, na kuelekeza nyuso zao juu;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu watatangatanga katika inchi, wenye kufazaika sana na wenye njaa. Na wakiwa na njaa, watakasirika na kumulaani mufalme wao vilevile na Mungu wao. Wataangalia juu mbinguni