Isaiah 8:9 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Unganeni enyi watu wa mataifa nanyi mtafedheheshwa! Sikilizeni enyi nchi za mbali duniani! Jiwekeni tayari na kufedheheshwa; naam, kaeni tayari na kufedheheshwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Inueni ukelele wa vita, enyi mataifa, na mkavunjwevunjwe! Sikilizeni, enyi nyote nchi za mbali. Jiandaeni kwa vita, nanyi mkavunjwevunjwe! Jiandaeni kwa vita, nanyi mkavunjwevunjwe!
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Fanyeni ghasia, enyi kabila za watu, Nanyi mtavunjwa vipande vipande; Tegeni masikio, ninyi nyote wa nchi zilizo mbali; Jikazeni viuno, nanyi mtavunjwa vipande vipande; Jikazeni viuno, nanyi mtavunjwa vipande vipande.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Unganeni enyi watu wa mataifa nanyi mtafedheheshwa! Sikilizeni enyi nchi za mbali duniani! Jiwekeni tayari na kufedheheshwa; naam, kaeni tayari na kufedheheshwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Inueni kilio cha vita, enyi mataifa na mkavunjwevunjwe! Sikilizeni, enyi nyote nchi za mbali. Jiandaeni kwa vita, nanyi mkavunjwevunjwe! Jiandaeni kwa vita, nanyi mkavunjwevunjwe!
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Inueni kilio cha vita, enyi mataifa, na mkavunjwevunjwe! Sikilizeni, enyi nyote nchi za mbali. Jiandaeni kwa vita, nanyi mkavunjwevunjwe! Jiandaeni kwa vita, nanyi mkavunjwevunjwe!
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ungameni pamoja, enyi makabila ya watu, Nanyi mtavunjwa vipande vipande; Tegeni masikio, ninyi nyote wa nchi zilizo mbali; Jitahidini, nanyi mtavunjwa vipande vipande; Jitahidini, nanyi mtavunjwa vipande vipande.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Unganeni enyi watu wa mataifa nanyi mtafedheheshwa! Sikilizeni enyi nchi za mbali duniani! Jiwekeni tayari na kufedheheshwa; naam, kaeni tayari na kufedheheshwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kasirikeni, ninyi makabila ya watu, kalegeeni kwa kituko! Sikilizeni, nyote mkaao katika nchi za mbali! Jifungeni, kisha legeeni kwa kituko!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Fanyeni ghasia, enyi kabila za watu, Nanyi mtavunjwa vipande vipande; Tegeni masikio, ninyi nyote wa nchi zilizo mbali; Jikazeni viuno, nanyi mtavunjwa vipande vipande; Jikazeni viuno, nanyi mtavunjwa vipande vipande.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Muungane, enyi watu wa mataifa, na kufezeheshwa! Musikilize, enyi inchi za mbali katika dunia! Mujiweke tayari na kufezeheshwa. Mujiweke tayari na kufezeheshwa.