Isaiah 9:12 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Waaramu upande wa mashariki, Wafilisti upande wa magharibi, wamepanua vinywa vyao kuimeza Israeli. Hata hivyo, hasira yake haijatulia, bado ameunyosha mkono wake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Waaramu kutoka upande wa mashariki na Wafilisti kutoka upande wa magharibi wameila Israeli kwa kinywa kilichopanuliwa. Hata kwa haya yote, hasira yake haijageukia mbali, mkono wake bado umeinuliwa juu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Waashuri upande wa mbele, na Wafilisti upande wa nyuma, nao watamla Israeli kwa kinywa kilicho wazi. Pamoja na hayo yote hasira yake haikugeukia mbali, lakini mkono wake umenyoshwa hata sasa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Waaramu upande wa mashariki, Wafilisti upande wa magharibi, wamepanua vinywa vyao kuimeza Israeli. Hata hivyo, hasira yake haijatulia, bado ameunyosha mkono wake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Waashuru kutoka upande wa mashariki na Wafilisti kutoka upande wa magharibi wameila Israeli kwa kinywa kilichopanuliwa. Hata kwa haya yote, hasira yake haijageukia mbali, mkono wake bado umeinuliwa juu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Waashuru kutoka upande wa mashariki na Wafilisti kutoka upande wa magharibi wameila Israeli kwa kinywa kilichopanuliwa. Hata kwa haya yote, hasira yake haijageukia mbali, mkono wake bado umeinuliwa juu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Waashuri upande wa mbele, na Wafilisti upande wa nyuma, nao watamla Israeli kwa kinywa kilicho wazi. Pamoja na hayo yote hasira yake haikugeukia mbali, lakini mkono wake umenyoshwa hata sasa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Waaramu upande wa mashariki, Wafilisti upande wa magharibi, wamepanua vinywa vyao kuimeza Israeli. Hata hivyo, hasira yake haijatulia, bado ameunyosha mkono wake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
upande wa mbele wakaja Waasuri upande wa nyuma Wafilisti, wakawala Waisiraeli na kuasama vinywa kabisa. Lakini kwa hayo yote makali yake hayajatulia bado, nao mkono wake ungaliko umekunjuka.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Waashuri upande wa mbele, na Wafilisti upande wa nyuma, nao watamla Israeli kwa kinywa kilicho wazi. Pamoja na hayo yote hasira yake haikugeukia mbali, lakini mkono wake umenyoshwa hata sasa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ingawa aliwaazibu watu, hawakumurudilia Yawe wa majeshi.