Isaiah 9:19 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa ghadhabu ya Mwenyezi-Mungu wa majeshi nchi imechomwa moto, na watu ni kama kuni za kuuwasha. Hakuna mtu anayemhurumia ndugu yake;
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hasira ya Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni nchi itachomwa kwa moto, nao watu watakuwa kuni za kuchochea moto. Hakuna mtu atakayemhurumia ndugu yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa sababu ya hasira ya Bwana wa majeshi nchi hii inateketea kabisa; watu hawa nao ni kama kuni zitiwazo motoni; hapana mtu amhurumiaye ndugu yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa ghadhabu ya Mwenyezi-Mungu wa majeshi nchi imechomwa moto, na watu ni kama kuni za kuuwasha. Hakuna mtu anayemhurumia ndugu yake;
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hasira ya BWANA Mwenye Nguvu Zote nchi itachomwa kwa moto, nao watu watakuwa kuni za kuchochea moto, hakuna mtu atakayemhurumia ndugu yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hasira ya bwana Mwenye Nguvu Zote nchi itachomwa kwa moto, nao watu watakuwa kuni za kuchochea moto. Hakuna mtu atakayemhurumia ndugu yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa sababu ya hasira ya BWANA wa majeshi nchi hii inateketea kabisa; watu hawa nao ni kama kuni zitiwazo motoni; hapana mtu amhurumiaye ndugu yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa ghadhabu ya Mwenyezi-Mungu wa majeshi nchi imechomwa moto, na watu ni kama kuni za kuuwasha. Hakuna mtu anayemhurumia ndugu yake;
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nchi ikateketea kwa moto wa makali ya Bwana Mwenye vikosi, watu wakawa kama chakula cha moto, kwa hiyo hakuwako aliyemwonea ndugu yake uchungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa sababu ya hasira ya BWANA wa majeshi nchi hii inateketea kabisa; watu hawa nao ni kama kuni zitiwazo motoni; hapana mtu amhurumiaye ndugu yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
wananyanganya upande mumoja na hawatosheki; wanakula upande mwingine lakini hawashibi. Kila mumoja anamushambulia mwenzake.