Isaiah 9:20 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
wananyanganya upande mmoja na hawatosheki; wanakula upande mwingine lakini hawashibi. Kila mmoja anamshambulia mwenzake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Upande wa kuume watakuwa wakitafuna, lakini bado wataona njaa; upande wa kushoto watakuwa wakila, lakini hawatashiba. Kila mmoja atajilisha kwa nyama ya uzao wake mwenyewe:
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hupokonya upande wa mkono wa kuume, nao huona njaa! Hula upande wa mkono wa kushoto, wala hawashibi! Watakula kila mtu nyama ya mkono wake mwenyewe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
wananyang'anya upande mmoja na hawatosheki; wanakula upande mwingine lakini hawashibi. Kila mmoja anamshambulia mwenzake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Upande wa kuume watakuwa wakitafuna, lakini bado wataona njaa; upande wa kushoto watakuwa wakila, lakini hawatashiba. Kila mmoja atajilisha kwa nyama ya mtoto wake mwenyewe:
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Upande wa kuume watakuwa wakitafuna, lakini bado wataona njaa; upande wa kushoto watakuwa wakila, lakini hawatashiba. Kila mmoja atajilisha kwa nyama ya mtoto wake mwenyewe:
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hupokonya upande wa mkono wa kulia, nao huona njaa! Hula upande wa mkono wa kushoto, wala hawashibi! Watakula kila mtu nyama ya mkono wake mwenyewe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
wananyanganya upande mmoja na hawatosheki; wanakula upande mwingine lakini hawashibi. Kila mmoja anamshambulia mwenzake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakajikatia kuumeni, lakini njaa haikuondoka; wakala nako kushotoni, lakini hawakushiba; kisha wakala kila mtu nyama ya mkono wake:
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hupokonya upande wa mkono wa kuume, nao huona njaa! Hula upande wa mkono wa kushoto, wala hawashibi! Watakula kila mtu nyama ya mkono wake mwenyewe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Manase anashambulia Efuraimu, Efuraimu anashambulia Manase na wote wawili wanashambulia Yuda. Hata hivyo, hasira ya Yawe haijatulia, angali ananyoosha mukono wake kwa kuwaazibu.