Isaiah 9:21 — Compare Translations
10 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Manase dhidi ya Efraimu, Efraimu dhidi ya Manase na wote wawili dhidi ya Yuda. Hata hivyo, hasira ya Mwenyezi-Mungu haijatulia, bado ameunyosha mkono wake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Manase atamla Efraimu, naye Efraimu atamla Manase; nao pamoja watakuwa kinyume na Yuda. Hata kwa haya yote, hasira yake haijageukia mbali, mkono wake bado umeinuliwa juu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Manase anamla Efraimu, naye Efraimu anamla Manase; nao wawili pamoja watakuwa juu ya Yuda. Pamoja na hayo yote hasira yake haikugeukia mbali, lakini mkono wake umenyoshwa hata sasa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Manase dhidi ya Efraimu, Efraimu dhidi ya Manase na wote wawili dhidi ya Yuda. Hata hivyo, hasira ya Mwenyezi-Mungu haijatulia, bado ameunyosha mkono wake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Manase atamla Efraimu, naye Efraimu atamla Manase; kwa pamoja watakuwa kinyume na Yuda. Hata kwa haya yote, hasira yake haijageukia mbali, mkono wake bado umeinuliwa juu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Manase atamla Efraimu, naye Efraimu atamla Manase; nao pamoja watakuwa kinyume na Yuda. Hata kwa haya yote, hasira yake haijageukia mbali, mkono wake bado umeinuliwa juu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Manase anamla Efraimu, naye Efraimu anamla Manase; nao wawili pamoja watakuwa juu ya Yuda. Pamoja na hayo yote hasira yake haikugeukia mbali, lakini mkono wake umenyoshwa hata sasa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Manase dhidi ya Efraimu, Efraimu dhidi ya Manase na wote wawili dhidi ya Yuda. Hata hivyo, hasira ya Mwenyezi-Mungu haijatulia, bado ameunyosha mkono wake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Manase akamla Efuraimu, naye Efuraimu akamla Manase, kisha wote wawili pamoja wakamgeukia Yuda. Lakini kwa hayo yote makali yake hayajatulia bado, nao mkono wake ungaliko umekunjuka.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)