Isaiah 9:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Viatu vyote vya washambulizi vitani na mavazi yote yenye madoa ya damu yatateketezwa kama kuni za kuwasha moto.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kila kiatu cha shujaa kilichotumiwa vitani, na kila vazi lililovingirishwa katika damu vitawekwa kwa ajili ya kuchomwa, vitakuwa kuni za kuwasha moto.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana silaha zote za mtu mwenye silaha wakati wa mshindo, na mavazi yaliyofingirishwa katika damu, yatakuwa tayari kuteketezwa, yatakuwa kuni za kutiwa motoni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Viatu vyote vya washambulizi vitani na mavazi yote yenye madoa ya damu yatateketezwa kama kuni za kuwasha moto.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kila kiatu cha askari kilichotumiwa vitani na kila vazi lililovingirishwa katika damu litawekwa kwa ajili ya kuchomwa, vitakuwa kuni za kuwasha moto.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kila kiatu cha askari kilichotumiwa vitani, na kila vazi lililovingirishwa katika damu vitawekwa kwa ajili ya kuchomwa, vitakuwa kuni za kuwasha moto.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana silaha zote za mtu mwenye silaha wakati wa mshindo, na mavazi yaliyovingirishwa katika damu, yatakuwa tayari kuteketezwa, yatakuwa kuni za kutiwa motoni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Viatu vyote vya washambulizi vitani na mavazi yote yenye madoa ya damu yatateketezwa kama kuni za kuwasha moto.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani mata yote, waliyoyashika kwenye mapigano, nazo nguo zilizofuliwa katika damu zitateketezwa kwa ukali wa moto.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana silaha zote za mtu mwenye silaha wakati wa mshindo, na mavazi yaliyofingirishwa katika damu, yatakuwa tayari kuteketezwa, yatakuwa kuni za kutiwa motoni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Maana mutoto amezaliwa kwa ajili yetu, tumepewa mutoto mwanaume. Naye atapewa mamlaka ya kutawala. Ataitwa: “Mushauri wa Ajabu”, “Mungu Mwenye Nguvu”, “Baba wa Milele”, “Mufalme wa Amani”.