James 1:27 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Dini iliyo safi na isiyo na hitilafu mbele ya Mungu Baba ni hii: Kuwasaidia yatima na wajane katika shida zao, na kujilinda mwenyewe usichafuliwe na ulimwengu huu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Dini iliyo safi, isiyo na uchafu, inayokubalika mbele za Mungu, Baba yetu, ndiyo hii: ni kuwasaidia yatima na wajane katika dhiki zao na kujilinda usitiwe madoa na dunia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Dini safi na isiyo na lawama mbele za Mungu Baba, inahusisha haya: kuwatunza yatima na wajane katika mazingira mgumu na kujilinda asichafuliwe na ulimwengu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Dini iliyo safi na isiyo na hitilafu mbele ya Mungu Baba ni hii: Kuwasaidia yatima na wajane katika shida zao, na kujilinda mwenyewe usichafuliwe na ulimwengu huu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Dini iliyo safi na isiyo na hitilafu mbele ya Mungu Baba ni hii: Kuwasaidia yatima na wajane katika shida zao, na kujilinda mwenyewe usichafuliwe na ulimwengu huu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Dini iliyo safi, isiyo na uchafu, inayokubalika mbele za Mungu Baba yetu, ndiyo hii: Kuwasaidia yatima na wajane katika dhiki zao na kujilinda usitiwe madoa na dunia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Dini iliyo safi, isiyo na uchafu, inayokubalika mbele za Mungu Baba yetu, ndiyo hii: Kuwasaidia yatima na wajane katika dhiki zao na kujilinda usitiwe madoa na dunia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Dini iliyo safi, isiyo na dosari mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Dini iliyo safi na isiyo na hitilafu mbele ya Mungu Baba ni hii: Kuwasaidia yatima na wajane katika shida zao, na kujilinda mwenyewe usichafuliwe na ulimwengu huu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Matumikio yatakatayo yasiyo yenye doa hata machoni pa Mungu Baba ndiyo haya: kukagua watoto waliofiwa na wazazi na kukagua nao wanawake wajane katika maumivu yao na kujilinda wenyewe, tusijitie katika machafu ya ulimwwengu huu.*
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Dini inayokuwa safi na bila kosa mbele ya Mungu Baba ndiyo hii: kushugulikia wayatima na wajane wanaoteswa, na kujilinda mwenyewe na uchafu wa dunia hii.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Dini iliyo safi na isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika shidda yao, na kujilinda pasipo mawaa katika dunia.