James 1:4 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Muwe na hakika kwamba uvumilivu wenu utawategemeza mpaka mwisho, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu, bila kupungukiwa chochote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Acheni saburi ikamilishe kazi yake, ili mpate kuwa wakamilifu na watimilifu, bila kupungukiwa chochote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Saburi na iwe na kazi kamilifu, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu bila kupungukiwa na neno.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Na uvumilivu unapaswa kukamilisha kazi yake, ili kwamba muwe watu waliokomaa na wakamilifu msiopungukiwa na kitu cho chote.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Muwe na hakika kwamba uvumilivu wenu utawategemeza mpaka mwisho, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu, bila kupungukiwa chochote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Muwe na hakika kwamba uvumilivu wenu utawategemeza mpaka mwisho, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu, bila kupungukiwa chochote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Saburi na iwe na kazi timilifu, ili mpate kuwa wakamilifu, mmekamilishwa, bila kupungukiwa na kitu cho chote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Saburi na iwe na kazi timilifu, ili mpate kuwa wakamilifu, mmekamilishwa, bila kupungukiwa na kitu chochote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Saburi na iwe na kazi kamilifu, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu bila kupungukiwa na neno.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Muwe na hakika kwamba uvumilivu wenu utawategemeza mpaka mwisho, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu, bila kupungukiwa chochote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao uvumilivu sharti uitimize kazi yake, ninyi mpate kutimilika, mwe Wakristo wazima wasioachwa nyuma katika jambo lo lote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Saburi na iwe na kazi kamilifu, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu bila kupungukiwa na neno.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini sherti uvumilivu ule utimize kazi yake, kusudi mupate kuwa wakamilifu na watimilifu wasiopungukiwa na kitu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na saburi iwe na kazi kamilifu, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu bila kupungukiwa neno.