James 2:16 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yafaa kitu gani nyinyi kuwaambia hao: “Nendeni salama mkaote moto na kushiba,” bila kuwapatia mahitaji yao ya maisha?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
naye mmoja wenu akamwambia, “Nenda zako kwa amani, ukaote moto na kushiba,” pasipo kumpatia yale mahitaji ya mwili aliyopungukiwa, yafaa nini?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na mtu wa kwenu akawaambia, Enendeni zenu kwa amani, mkaote moto na kushiba, lakini asiwape mahitaji ya mwili, yafaa nini?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
na ukawaambia, “Mungu awe nanyi! Mkahifadhiwe mahala pa joto na mle vizuri!” Hiyo ina manufaa gani kwao? Usipowapa vitu wanavyovihitaji, maneno yako yanakosa maana!
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yafaa kitu gani ninyi kuwaambia hao: “Nendeni salama mkaote moto na kushiba,” bila kuwapatia mahitaji yao ya maisha?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yafaa kitu gani nyinyi kuwaambia hao: “Nendeni salama mkaote moto na kushiba,” bila kuwapatia mahitaji yao ya maisha?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
mmoja wenu akamwambia, “Enenda zako kwa amani, ukaote moto na kushiba,” pasipo kumpatia yale mahitaji ya mwili aliyopungukiwa, yafaa nini?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
mmoja wenu akamwambia, “Enenda zako kwa amani, ukaote moto na kushiba,” pasipo kumpatia yale mahitaji ya mwili aliyopungukiwa, yafaa nini?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na mmoja wenu akawaambia, Nendeni zenu kwa amani, mkaote moto na kushiba, lakini asiwape mahitaji ya kimwili, yafaa nini?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yafaa kitu gani nyinyi kuwaambia hao: “Nendeni salama mkaote moto na kushiba,” bila kuwapatia mahitaji yao ya maisha?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
mtu wa kwenu akawaambia: Nendeni na kutengemana, mwote moto, mpate kushiba! asiwape yaipasayo miili yao, itawafaliaje?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na mtu wa kwenu akawaambia, Enendeni zenu kwa amani, mkaote moto na kushiba, lakini asiwape mahitaji ya mwili, yafaa nini?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
itakuwa na faida gani, kama mumoja wenu anamwambia: “Mwende vizuri, mukaote moto na kushiba,” lakini hamusaidii na kitu chochote?
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
mtu wa kwenu akawaambia, Enendeni zenu kwa amani, mkaote moto na kushiba, illakini asiwape mahitaji ya mwili, yafaa nini?