James 2:23 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hivyo yakatimia yale Maandiko Matakatifu yasemayo: “Abrahamu alimwamini Mungu, na kwa imani yake akakubaliwa kuwa mtu mwadilifu; na hivyo Abrahamu akaitwa rafiki ya Mungu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa njia hiyo likatimizwa andiko lisemalo, “Ibrahimu alimwamini Mungu, na ikahesabiwa kwake kuwa haki,” naye akaitwa rafiki wa Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maandiko yale yakatimizwa yaliyonena, Ibrahimu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa ni haki; naye aliitwa rafiki wa Mungu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ndipo yakatimizwa yale yaliyo kwenye Maandiko kuwa, “Ibrahimu alimwamini Mungu, na kwa imani hiyo akafanywa kuwa mwenye haki kwa Mungu,” na kwa sababu hiyo akaitwa “Rafiki wa Mungu”.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hivyo yakatimia yale Maandiko Matakatifu yasemayo: “Abrahamu alimwamini Mungu na kwa imani yake akakubaliwa kuwa mtu mwadilifu; na hivyo Abrahamu akaitwa rafiki wa Mungu.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hivyo yakatimia yale Maandiko Matakatifu yasemayo: “Abrahamu alimwamini Mungu, na kwa imani yake akakubaliwa kuwa mtu mwadilifu; na hivyo Abrahamu akaitwa rafiki ya Mungu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa njia hiyo yakatimizwa yale Maandiko yasemayo, “Abrahamu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa haki,” naye akaitwa rafiki wa Mungu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa njia hiyo yakatimizwa yale Maandiko yasemayo, “Ibrahimu alimwamini Mwenyezi Mungu na ikahesabiwa kwake kuwa haki,” naye akaitwa rafiki wa Mwenyezi Mungu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maandiko yale yakatimizwa yaliyonena, Abrahamu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa ni haki; naye aliitwa rafiki wa Mungu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hivyo yakatimia yale Maandiko Matakatifu yasemayo: “Abrahamu alimwamini Mungu, na kwa imani yake akakubaliwa kuwa mtu mwadilifu; na hivyo Abrahamu akaitwa rafiki ya Mungu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
nayo yaliyoandikwa yakatimia kwamba: Aburahamu alimtegemea Mungu, kwa hiyo akawaziwa kuwa mwenye wongofu, akaitwa mpenzi wake Mungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maandiko yale yakatimizwa yaliyonena, Ibrahimu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa ni haki; naye aliitwa rafiki wa Mungu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na maandiko haya yakatimia: “Abrahamu alimwamini Mungu na kwa hiyo akahesabiwa kuwa mwenye haki.” Na Mungu akamwita rafiki yake.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maandiko yale yakatimizwa yaliyonena, Ibrahimu alimwamini Mungu ikahesabiwa kwake kuwa ni haki: nae aliitwa raliki wa Mungu.