James 2:25 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ilikuwa vivyo hivyo kuhusu yule malaya Rahabu; yeye alikubaliwa kuwa mwadilifu kwa sababu aliwapokea wale wapelelezi na kuwasaidia waende zao kwa kupitia njia nyingine.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Vivyo hivyo, hata Rahabu, yule kahaba: je, hakuhesabiwa haki kwa yale aliyotenda alipowapokea wale wapelelezi na kuwaambia waende njia nyingine?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Vivyo hivyo na Rahabu, yule kahaba naye, je! Hakuhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo, hapo alipowakaribisha wajumbe, akawatoa nje kwa njia nyingine?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Je, Rahabu yule kahaba si alifanywa kuwa mwenye haki na Mungu kwa matendo aliyofanya, alipowasaidia wale waliokuwa wakipeleleza nchi kwa niaba ya watu wa Mungu. Aliwakaribisha nyumbani mwake na kuwawezesha kutoroka kwa njia nyingine.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ilikuwa vivyo hivyo kuhusu yule malaya Rahabu; yeye alikubaliwa kuwa mwadilifu kwa sababu aliwapokea wale wapelelezi na kuwasaidia waende zao kwa kupitia njia nyingine.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ilikuwa vivyo hivyo kuhusu yule malaya Rahabu; yeye alikubaliwa kuwa mwadilifu kwa sababu aliwapokea wale wapelelezi na kuwasaidia waende zao kwa kupitia njia nyingine.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Vivyo hivyo, hata Rahabu, yule kahaba, hakuhesabiwa haki kwa yale aliyotenda alipowapokea wale wapelelezi na kuwaambia waende njia nyingine?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Vivyo hivyo, hata Rahabu, yule kahaba, hakuhesabiwa haki kwa yale aliyotenda alipowapokea wale wapelelezi na kuwaambia waende njia nyingine?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Vivyo hivyo na Rahabu, yule kahaba naye, je! Hakuhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo, hapo alipowakaribisha wajumbe, akawatoa nje kwa njia nyingine?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ilikuwa vivyo hivyo kuhusu yule malaya Rahabu; yeye alikubaliwa kuwa mwadilifu kwa sababu aliwapokea wale wapelelezi na kuwasaidia waende zao kwa kupitia njia nyingine.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena je? Yule mke mgoni Rahabu hakupata wongofu naye kwa matendo, alipowafikiza wale wajumbe na kuwatoa mjini kwa njia nyingine?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Vivyo hivyo na Rahabu, yule kahaba naye, je! Hakuhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo, hapo alipowakaribisha wajumbe, akawatoa nje kwa njia nyingine?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ilikuwa hivi vilevile kwa yule kahaba Rahaba. Mungu alimuhesabia haki kwa njia ya matendo yake, wakati alipowakaribisha wapelelezi na kuwatorosha kwa njia nyingine.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na Rahab, yule kahaba nae, je! hakuhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo, alipowakaribisha wajumbe, akawatoa nje kwa njia nyingine?