James 2:3 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ikiwa mtamstahi zaidi yule aliyevaa mavazi ya kuvutia na kumwambia: “Keti hapa mahali pazuri,” na kumwambia yule maskini: “Wewe, simama huko,” au “Keti hapa sakafuni miguuni pangu,”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mkimpa heshima yule aliyevaa mavazi mazuri na kumwambia, “Keti hapa mahali pazuri,” lakini yule maskini mkamwambia, “Wewe simama pale,” au “Keti hapa sakafuni karibu na miguu yangu,”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
nanyi mkimstahi yule aliyevaa mavazi mazuri, na kumwambia, Keti wewe hapa mahali pazuri; na kumwambia yule maskini, Simama wewe pale, au keti miguuni pangu,
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Na tuchukulie kuwa mnaonyesha kumjali zaidi yule mtu aliyevaa mavazi mazuri na kusema, “Wewe keti hapa katika kiti hiki kizuri.” Lakini unamwambia yule mtu maskini, “Wewe simama pale,” au, “Keti chini karibu na miguu yetu.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ikiwa mtamstahi zaidi yule aliyevaa mavazi ya kuvutia na kumwambia: “Keti hapa mahali pazuri,” na kumwambia yule maskini: “Wewe, simama huko,” au “Keti hapa sakafuni miguuni pangu,”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ikiwa mtamstahi zaidi yule aliyevaa mavazi ya kuvutia na kumwambia: “Keti hapa mahali pazuri,” na kumwambia yule maskini: “Wewe, simama huko,” au “Keti hapa sakafuni miguuni pangu,”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
nanyi mkampa heshima yule aliyevaa mavazi mazuri na kumwambia, “Keti hapa mahali pazuri,” lakini yule maskini mkamwambia, “Wewe simama pale,” au “Keti hapa sakafuni karibu na miguu yangu,”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
nanyi mkampa heshima yule aliyevaa mavazi mazuri na kumwambia, “Keti hapa mahali pazuri,” lakini yule maskini mkamwambia, “Wewe simama pale,” au “Keti hapa sakafuni karibu na miguu yangu,”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
nanyi mkimstahi yule aliyevaa mavazi mazuri, na kumwambia, Wewe keti hapa mahali pazuri; na kumwambia yule maskini, Wewe simama pale, au keti miguuni pangu,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ikiwa mtamstahi zaidi yule aliyevaa mavazi ya kuvutia na kumwambia: “Keti hapa mahali pazuri,” na kumwambia yule maskini: “Wewe, simama huko,” au “Keti hapa sakafuni miguuni pangu,”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
nanyi mkamtazama yule aliyevaa mavazi mazuri na kumwambia: Wewe kaa hapa pazuri! kisha mkamwambia yule maskini: Wewe simama huko au kaa hapa chini miguuni pangu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
nanyi mkimstahi yule aliyevaa mavazi mazuri, na kumwambia, Keti wewe hapa mahali pazuri; na kumwambia yule maskini, Simama wewe pale, au keti miguuni pangu,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu munaonyesha heshima kwa yule anayevaa vizuri na kumwambia: “Ikaa hapa kwenye nafasi nzuri.” Lakini munamwambia yule masikini: “We! Simama pale, au uikae hapa chini kwenye nafasi ya kuwekea miguu yangu.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
nanyi mkimstahi yule aliyevaa mavazi mazuri, na kumwambia, Keti wewe hapa mahali pazuri, na kumwambia yule maskini, Simama wewe pale, au keti miguuni pangu,