James 3:13 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Je, ni nani mwenye hekima na akili miongoni mwenu? Basi, aoneshe jambo hilo kwa mwenendo wake mzuri na kwa matendo yake mema yanayofanyika kwa unyenyekevu na hekima.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ni nani aliye na hekima na ufahamu miongoni mwenu? Basi na aioneshe hiyo kwa maisha yake mema na kwa matendo yake yaliyotendwa kwa unyenyekevu utokanao na hekima.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
N'nani aliye na hekima na ufahamu kwenu? Na aonyeshe kazi zake kwa mwenendo wake mzuri, katika upole wa hekima.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Nani miongoni mwenu aliye na hekima na ufahamu? Na aoneshe hekima yake kwa mwenendo mzuri, kwa matendo yake yanayofanywa kwa unyenyekevu unaoletwa na hekima.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Je, ni nani mwenye hekima na akili miongoni mwenu? Basi, aonyeshe jambo hilo kwa mwenendo wake mzuri na kwa matendo yake mema yanayofanyika kwa unyenyekevu na hekima.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Je, ni nani mwenye hekima na akili miongoni mwenu? Basi, aoneshe jambo hilo kwa mwenendo wake mzuri na kwa matendo yake mema yanayofanyika kwa unyenyekevu na hekima.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ni nani aliye na hekima na ufahamu miongoni mwenu? Basi na aionyeshe hiyo kwa maisha yake mema na kwa matendo yake yaliyotendwa kwa unyenyekevu utokanao na hekima.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ni nani aliye na hekima na ufahamu miongoni mwenu? Basi na aionyeshe hiyo kwa maisha yake mema na kwa matendo yake yaliyotendwa kwa unyenyekevu utokanao na hekima.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ni nani aliye na hekima na ufahamu kwenu? Na aonyeshe kazi zake kwa mwenendo wake mzuri, katika upole wa hekima.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Je, ni nani mwenye hekima na akili miongoni mwenu? Basi, aoneshe jambo hilo kwa mwenendo wake mzuri na kwa matendo yake mema yanayofanyika kwa unyenyekevu na hekima.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwenu yuko nani aliye mwerevu wa kweli wa kujua mambo? Ajionyeshe kuwa mwenye mwenendo mzuri, nazo kazi zake zijulike kuwa zenye upole utokao katika huo werevu wa kweli!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
N’nani aliye na hekima na ufahamu kwenu? Na aonyeshe kazi zake kwa mwenendo wake mzuri, katika upole wa hekima.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nani anayekuwa na hekima na ufahamu kati yenu? Basi aonyeshe jambo lile kwa njia ya mwenendo wake muzuri, kwa njia ya matendo yanayofanyika katika upole unaotokana na hekima ile.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nani aliye na hekima na fahamu kwenu? Na aonyeshe kazi zake kwa mwenendo wake mzuri, katika upole wa hekima.