James 3:17 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini hekima itokayo juu mbinguni, kwanza ni safi; inapenda amani, upole na huwajali watu; imejaa huruma na huzaa matunda ya matendo mema; haina ubaguzi wala unafiki.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini hekima inayotoka mbinguni kwanza ni safi, kisha inapenda amani, tena ni ya upole, iliyo tayari kusikiliza wengine kwa unyenyekevu, iliyojaa huruma na matunda mema, isiyopendelea mtu, tena isiyokuwa na unafiki.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina, haina unafiki.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini hekima inayotoka mbinguni juu kwanza juu ya yote ni safi, kisha ni ya amani ina upole na ina busara. Imejaa rehema na huzaa mavuno ya matendo mema. Haina upendeleo wala unafiki.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini hekima itokayo juu mbinguni, kwanza ni safi; inapenda amani, upole na huwajali watu; imejaa huruma na huzaa matunda ya matendo mema; haina ubaguzi wala unafiki.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini hekima itokayo juu mbinguni, kwanza ni safi; inapenda amani, upole na huwajali watu; imejaa huruma na huzaa matunda ya matendo mema; haina ubaguzi wala unafiki.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini hekima itokayo mbinguni kwanza ni safi, kisha inapenda amani, ya upole, iliyo tayari kusikiliza maneno ya watu wengine, yenye unyenyekevu, iliyojaa huruma na matunda mema, isiyopendelea mtu, tena isiyokuwa na unafiki.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini hekima itokayo mbinguni kwanza ni safi, kisha inapenda amani, tena ni ya upole, iliyo tayari kusikiliza wengine kwa unyenyekevu, iliyojaa huruma na matunda mema, isiyopendelea mtu, tena isiyokuwa na unafiki.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina, haina unafiki.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini hekima itokayo juu mbinguni, kwanza ni safi; inapenda amani, upole na huwajali watu; imejaa huruma na huzaa matunda ya matendo mema; haina ubaguzi wala unafiki.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini werevu wa kweli utokao mbinguni juu kwanza ni wenye ung'avu, kisha ni wenye utengemano na upole na unyenyekevu, huwahurumia wote na kuwapatia mazao mema; haupendelei, maana hukataa ujanja.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina, haina unafiki.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini hekima inayotoka mbinguni, kwanza ni safi, tena ni yenye amani, upole na usikilivu, inajaa huruma na matendo mema. Haina upendeleo wala udanganyifu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole,, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina wala unafiki;