James 3:4 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Meli nazo pia, ingawa ni kubwa sana, na husukumwa na upepo mkali, huweza kugeuzwa kwa usukani mdogo sana, zikaelekea kokote nahodha anakotaka.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Au chukua mfano wa meli: ingawa ni kubwa sana, nazo hupelekwa na upepo mkali, zinaelekezwa kwa usukani mdogo sana kokote wanakotaka nahodha.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena angalieni merikebu; ingawa ni kubwa kama nini, na kuchukuliwa na pepo kali, zageuzwa na usukani mdogo sana, ko kote anakoazimia kwenda nahodha.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Au tuchukue meli kama mfano: Hata kama ni kubwa mno na husukumwa na upepo mkali, zinaongozwa kwa usukani mdogo sana na kwenda po pote alikokusudia nahodha kuipeleka.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Meli nazo pia, ingawa ni kubwa sana, na husukumwa na upepo mkali, huweza kugeuzwa kwa usukani mdogo sana, zikaelekea kokote nahodha anakotaka.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Meli nazo pia, ingawa ni kubwa sana, na husukumwa na upepo mkali, huweza kugeuzwa kwa usukani mdogo sana, zikaelekea kokote nahodha anakotaka.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Au angalia pia meli, ingawa ni kubwa sana, nazo huchukuliwa na upepo mkali, lakini hugeuzwa kwa usukani mdogo sana, ko kote anakotaka nahodha.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Au angalia pia meli, ingawa ni kubwa sana, nazo huchukuliwa na upepo mkali, lakini hugeuzwa kwa usukani mdogo sana, kokote anakotaka nahodha.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena angalieni merikebu; ingawa ni kubwa kama nini, na kuchukuliwa na pepo kali, zageuzwa na usukani mdogo sana, kokote anakoazimia kwenda nahodha.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Meli nazo pia, ingawa ni kubwa sana, na husukumwa na upepo mkali, huweza kugeuzwa kwa usukani mdogo sana, zikaelekea kokote nahodha anakotaka.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tazameni, hata merikebu zilivyo kubwa sana, tena zinavyochukuliwa na pepo zenye nguvu! Nazo huongozwa na sukani iliyo ndogo sana, mwenye kuishika anakotaka.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena angalieni merikebu; ingawa ni kubwa kama nini, na kuchukuliwa na pepo kali, zageuzwa na usukani mdogo sana, ko kote anakoazimia kwenda nahodha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Muangalie vilevile mashua. Hata mashua ni kubwa sana na zenye kusukumwa na upepo mukali, zinaongozwa na usukani mudogo sana na kuendeshwa pahali kapiteni anapotaka.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kaziangalieni merikebu; ingawa ni kubwua namna gani, na kuchukuliwa na pepo kali, zageuzwa na usukani mdogo sana, ko kote aazimuko kwenda yule aongozae.