James 3:5 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Vivyo hivyo, ulimi, ingawa ni kiungo kidogo cha mwili, hujisifia makuu sana. Moto mdogo waweza kuteketeza msitu mkubwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Vivyo hivyo ulimi ni kiungo kidogo sana katika mwili, lakini hujivuna majivuno makuu. Fikirini jinsi moto mdogo unavyoweza kuteketeza msitu mkubwa!
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Vivyo hivyo ulimi nao ni kiungo kidogo, nao hujivuna majivuno makuu. Angalieni jinsi moto mdogo uwashavyo msitu mkubwa sana.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kwa jinsi hiyo hiyo, ulimi ni kiungo kidogo sana katika mwili, lakini unaweza kujivuna kuwa umetenda mambo makubwa sana. Fikiri jinsi ambavyo msitu mkubwa unaweza kuwashwa moto kwa mwali mdogo tu!
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Vivyo hivyo, ulimi, ingawa ni kiungo kidogo cha mwili, hujisifia makuu sana. Moto mdogo waweza kuteketeza msitu mkubwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Vivyo hivyo, ulimi, ingawa ni kiungo kidogo cha mwili, hujisifia makuu sana. Moto mdogo waweza kuteketeza msitu mkubwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Vivyo hivyo ulimi ni kiungo kidogo sana katika mwili, lakini hujivuna majivuno makuu. Fikirini jinsi moto mdogo unavyoweza kuteketeza msitu mkubwa!
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Vivyo hivyo ulimi ni kiungo kidogo sana katika mwili, lakini hujivuna majivuno makuu. Fikirini jinsi moto mdogo unavyoweza kuteketeza msitu mkubwa!
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Vivyo hivyo ulimi nao ni kiungo kidogo, nao hujivunia matendo makuu. Angalieni jinsi moto mdogo uwashavyo msitu mkubwa sana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Vivyo hivyo, ulimi, ingawa ni kiungo kidogo cha mwili, hujisifia makuu sana. Moto mdogo waweza kuteketeza msitu mkubwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Vivyo hivyo nao ulimi ni kiungo kidogo, nao hujivunia makuu! Tazameni, moto ulio mdogo huchoma pori kubwa!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Vivyo hivyo ulimi nao ni kiungo kidogo, nao hujivuna majivuno makuu. Angalieni jinsi moto mdogo uwashavyo msitu mkubwa sana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hivi vilevile ulimi ni kiungo kidogo cha mwili, lakini unaweza kujivunia mambo makubwa sana. Muangalie, moto kidogo inaweza kuchoma pori kubwa sana!
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Vivyo hivyo ulimi nao ni kiungo kidogo, na hujivuna majivuno makuu.