James 3:6 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hali kadhalika ulimi ni kama moto. Umejaa maovu chungu nzima, unayo nafasi yake katika miili yetu na hueneza ubaya katika nafsi zetu zote. Huteketeza maisha yetu yote kwa moto utokao Jehanamu kwenyewe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ulimi pia ni moto, ndio ulimwengu wa uovu kati ya viungo vya mwili. Ulimi huutia mwili wote wa mtu unajisi na kuuwasha moto mfumo mzima wa maisha yake, nao wenyewe huchomwa moto wa Jehanamu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao ulimi ni moto; ule ulimwengu wa uovu, ule ulimi, umewekwa katika viungo vyetu, nao ndio uutiao mwili wote unajisi, huuwasha moto mfulizo wa maumbile, nao huwashwa moto na jehanum.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ndiyo, ulimi ni mwali wa moto. Ulimi unawakilisha ulimwengu wa uovu miongoni mwa viungo vya mwili wetu. Ulimi huo huo huuchafua mwili wote, na unaweza kuwasha moto maisha yote ya mtu. Nao unapata moto wake kutoka Jehanamu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hali kadhalika ulimi ni kama moto. Umejaa maovu chungu nzima, unayo nafasi yake katika miili yetu na hueneza ubaya katika nafsi zetu zote. Huteketeza maisha yetu yote kwa moto utokao Jehanamu kwenyewe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hali kadhalika ulimi ni kama moto. Umejaa maovu chungu nzima, unayo nafasi yake katika miili yetu na hueneza ubaya katika nafsi zetu zote. Huteketeza maisha yetu yote kwa moto utokao Jehanamu kwenyewe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ulimi pia ni moto, ndio ulimwengu wa uovu kati ya viungo vya mwili. Ulimi huutia mwili wote wa mtu unajisi na kuuwasha moto mfumo mzima wa maisha yake, nao wenyewe huchomwa moto wa jehanamu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ulimi pia ni moto, ndio ulimwengu wa uovu kati ya viungo vya mwili. Ulimi huutia mwili wote wa mtu unajisi na kuuwasha moto mfumo mzima wa maisha yake, nao wenyewe huchomwa moto wa Jehanamu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao ulimi ni moto; ule ulimwengu wa uovu, ule ulimi, umewekwa katika viungo vyetu, nao ndio uutiao mwili wote unajisi, huuwasha moto mfululizo wa maumbile, nao huwashwa moto na Jehanamu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hali kadhalika ulimi ni kama moto. Umejaa maovu chungu nzima, unayo nafasi yake katika miili yetu na hueneza ubaya katika nafsi zetu zote. Huteketeza maisha yetu yote kwa moto utokao Jehanamu kwenyewe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao ulimi ni moto, ni ulimwengu wenye upotovu. Katika viungo vyetu ndio ulimi unaouchafua mwili wote, unavichoma vyote vilivyoumbwa, wenyewe ukiwashwa na moto ulioko kuzimuni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao ulimi ni moto; ule ulimwengu wa uovu, ule ulimi, umewekwa katika viungo vyetu, nao ndio uutiao mwili wote unajisi, huuwasha moto mfulizo wa maumbile, nao huwashwa moto na jehanum.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nao ulimi ni kama moto. Ulimi ni kiungo kinachojaa ubaya wa kila namna. Ulimi unapatikana kwenye nafasi yake katikati ya viungo vyetu, nao ndio unaochafua mwili wote. Unateketeza maisha yetu ukichomwa wenyewe na moto unaotoka katika jehenamu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kaangalieni jinsi moto mdogo uwasbavyo kuni nyingi sana. Nao ulimi ni moto, ulimwengu wa uovu. Ndio khabari ya ulimi katika viungo vyetu, huutia najis mwili wote, huliwasha moto gurudumu la maumbile, nao huwashwa moto na jehannum.