James 3:9 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa ulimi sisi twamshukuru Bwana na Baba yetu. Kwa ulimi huhuo twawalaani watu, watu ambao wameumbwa kwa mfano wa Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa ulimi tunamhimidi Mwenyezi Mungu na Baba yetu, na kwa huo twawalaani watu walioumbwa kwa mfano wa Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa huo twamhimidi Mungu Baba yetu, na kwa huo twawalaani wanadamu waliofanywa kwa mfano wa Mungu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kwa ulimi huo tunambariki Bwana na Baba, na kwa huo huo tunawalaani watu walioumbwa kwa mfano wa Mungu!
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kwa ulimi sisi twamshukuru Bwana na Baba yetu. Kwa ulimi huohuo twawalaani watu, watu ambao wameumbwa kwa mfano wa Mungu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa ulimi sisi twamshukuru Bwana na Baba yetu. Kwa ulimi huhuo twawalaani watu, watu ambao wameumbwa kwa mfano wa Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa ulimi tunamhimidi Bwana, yaani, Baba yetu na kwa huo twawalaani watu walioumbwa kwa mfano wa Mungu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa ulimi tunamhimidi Bwana Mwenyezi, yaani Baba yetu, na kwa huo twawalaani watu walioumbwa kwa mfano wa Mwenyezi Mungu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa huo tunamhimidi Mungu Baba yetu, na kwa huo tunawalaani wanadamu walioumbwa kwa mfano wa Mungu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa ulimi sisi twamshukuru Bwana na Baba yetu. Kwa ulimi huhuo twawalaani watu, watu ambao wameumbwa kwa mfano wa Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndio, unaotutukuzisha Bwana aliye Baba, tena ndio, unaotuapizisha watu walioumbwa kwa mfano wa Mungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa huo twamhimidi Mungu Baba yetu, na kwa huo twawalaani wanadamu waliofanywa kwa mfano wa Mungu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa njia ya ulimi tunamusifu Bwana anayekuwa Baba yetu, na kwa njia ile ile tunalaani watu walioumbwa kwa mufano wa Mungu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa huo twamhimidi Mungu Baba yetu, na kwa huo twawalaani wana Adamu waliofanywa kwa mfano wa Mungu.