James 4:11 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndugu, msilaumiane nyinyi kwa nyinyi. Anayemlaumu ndugu yake na kumhukumu, huyo huilaumu na kuihukumu sheria. Kama ukiihukumu sheria, basi, wewe huitii sheria, bali waihukumu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndugu, msineneane mabaya ninyi kwa ninyi. Mtu yeyote anayesema mabaya dhidi ya ndugu yake au kumhukumu, anasema dhidi ya sheria na kuihukumu. Unapoihukumu sheria, basi huishiki sheria, bali umekuwa hakimu wa kuihukumu hiyo sheria.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndugu, msisingiziane; amsingiziaye ndugu yake, au kumhukumu ndugu yake, huisingizia sheria na kuihukumu sheria. Lakini ukiihukumu sheria, huwi mtenda sheria, bali umekuwa hakimu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ndugu, msiendelee kukosoana ninyi kwa ninyi. Yeye anayemnenea mabaya ndugu yake au anayemhukumu ndugu yake atakuwa anailaumu Sheria na atakuwa anaihukumu Sheria. Na kama utaihukumu Sheria, hautakuwa unafanya yale yanayosemwa na Sheria, bali utakuwa ni hakimu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ndugu, msilaumiane ninyi kwa ninyi. Anayemlaumu ndugu yake na kumhukumu, huyo huilaumu na kuihukumu Sheria. Kama ukiihukumu Sheria, basi, wewe huitii Sheria, bali waihukumu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndugu, msilaumiane nyinyi kwa nyinyi. Anayemlaumu ndugu yake na kumhukumu, huyo huilaumu na kuihukumu sheria. Kama ukiihukumu sheria, basi, wewe huitii sheria, bali waihukumu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndugu, msineneane mabaya ninyi kwa ninyi. Mtu ye yote anayesema mabaya dhidi ya ndugu yake au kumhukumu anasema dhidi ya sheria na kuihukumu. Unapoihukumu sheria, basi huishiki sheria bali umekuwa hakimu wa kuihukumu hiyo sheria.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndugu, msineneane mabaya ninyi kwa ninyi. Mtu yeyote anayesema mabaya dhidi ya ndugu yake au kumhukumu anasema dhidi ya sheria na kuihukumu. Unapoihukumu sheria, basi huishiki sheria bali umekuwa hakimu wa kuihukumu hiyo sheria.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndugu, msisingiziane; amsingiziaye ndugu yake, au kumhukumu ndugu yake, huisingizia sheria na kuihukumu sheria. Lakini ukiihukumu sheria, huwi mtenda sheria, bali umekuwa hakimu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndugu, msilaumiane nyinyi kwa nyinyi. Anayemlaumu ndugu yake na kumhukumu, huyo huilaumu na kuihukumu sheria. Kama ukiihukumu sheria, basi, wewe huitii sheria, bali waihukumu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Msitetane, ndugu! Anayemteta ndugu au anayemwumbua ndugu yake huyateta Maonyo na kuyaumbua Maonyo. Lakini ukiyaumbua hu mfanyaji wa Maonyo, ila muumbuzi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndugu, msisingiziane; amsingiziaye ndugu yake, au kumhukumu ndugu yake, huisingizia sheria na kuihukumu sheria. Lakini ukiihukumu sheria, huwi mtenda sheria, bali umekuwa hakimu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wandugu, musisemeane ubaya. Yule anayesema ubaya juu ya ndugu yake au kumuhukumu, anasema ubaya juu ya Sheria na kuihukumu. Ukihukumu Sheria, wewe si mwenye kutii Sheria, lakini mwenye kuihukumu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Msisingiziane, ndugu; amsingiziae ndugu yake, au kumhukumu ndugu yake, aisingizia sharia na kuihukumu sharia. Lakini ukiihukumu sharia, huwi mtenda sharia, bali mhukumu.