James 4:14 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nyinyi hamjui hata maisha yenu yatakavyokuwa kesho! Nyinyi ni kama ukungu unaotokea kwa muda mfupi tu na kutoweka tena.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini hamjui hata litakalotukia kesho. Maisha yenu ni nini? Ninyi ni ukungu ambao huonekana kwa kitambo kidogo kisha hutoweka.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
walakini hamjui yatakayokuwako kesho. Uzima wenu ni nini? Maana ninyi ni mvuke uonekanao kwa kitambo, kisha hutoweka.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hamjui hata yatakayotokea katika maisha yenu kesho yake tu. Kwani ninyi ni mvuke tu ambao huonekana kwa kipindi kifupi tu kisha hutoweka.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ninyi hamjui hata maisha yenu yatakavyokuwa kesho! Ninyi ni kama ukungu unaotokea kwa muda mfupi tu na kutoweka tena.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nyinyi hamjui hata maisha yenu yatakavyokuwa kesho! Nyinyi ni kama ukungu unaotokea kwa muda mfupi tu na kutoweka tena.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini hamjui hata litakalotukia kesho. Maisha yenu ni nini? Ninyi ni ukungu ambao huonekana kwa kitambo kidogo kisha hutoweka.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini hamjui hata litakalotukia kesho. Maisha yenu ni nini? Ninyi ni ukungu ambao huonekana kwa kitambo kidogo kisha hutoweka.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
lakini hamjui yatakayokuwako kesho. Uzima wenu ni nini? Maana ninyi ni mvuke uonekanao kwa muda mfupi tu, kisha hutoweka.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nyinyi hamjui hata maisha yenu yatakavyokuwa kesho! Nyinyi ni kama ukungu unaotokea kwa muda mfupi tu na kutoweka tena.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nanyi hamjui, itakayokuwa kesho. Kuishi kwenu ni kwa namna gani? Maana ninyi m kama mvuke unaoonekana kitambo kidogo, kisha hutoweka.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
walakini hamjui yatakayokuwako kesho. Uzima wenu ni nini? Maana ninyi ni mvuke uonekanao kwa kitambo, kisha hutoweka.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ninyi hamujui namna gani maisha yenu yatakavyokuwa kesho! Kwa maana ninyi ni kama muvuke unaoonekana kwa wakati kidogo, kisha unatoweka.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Uzima wenu ni nini? Maana ninyi moshi uonekanao kwa kitambo, kiisha hutoweka.