James 4:6 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini, neema tunayopewa na Mungu ina nguvu zaidi; kama yasemavyo Maandiko: “Mungu huwapinga wenye majivuno lakini huwapa neema wanyenyekevu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini yeye hutupatia neema zaidi. Hii ndiyo sababu Maandiko yasema: “Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hiyo husema, Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini Mungu ametuonesha sisi, rehema kuu zaidi. Ndiyo maana Maandiko yanasema: Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa neema wale walio wanyenyekevu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini, neema tunayopewa na Mungu ina nguvu zaidi; kama yasemavyo Maandiko: “Mungu huwapinga wenye majivuno lakini huwapa neema wanyenyekevu.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini, neema tunayopewa na Mungu ina nguvu zaidi; kama yasemavyo Maandiko: “Mungu huwapinga wenye majivuno lakini huwapa neema wanyenyekevu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini yeye hutupatia neema zaidi. Hii ndiyo sababu Andiko husema: “Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini yeye hutupatia neema zaidi. Hii ndiyo sababu Andiko husema: “Mwenyezi Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hiyo husema, Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini, neema tunayopewa na Mungu ina nguvu zaidi; kama yasemavyo Maandiko: “Mungu huwapinga wenye majivuno lakini huwapa neema wanyenyekevu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nayo mema, atugawiayo, ni makubwa kuushinda. Kwa hiyo maandiko yasema: Wenye kujikweza Mungu huwapingia, lakini wanyenyekevu huwapatia huruma.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hiyo husema, Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Mungu ametujalia neema kubwa zaidi, kwa maana Maandiko yanasema: “Mungu anapingana na wenye kiburi, lakini anawajalia wanyenyekevu neema.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini atupa sisi neema nyingi zaidi; kwa hiyo asema, Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neemi wanyenyekevu.