James 5:12 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Zaidi ya hayo yote, ndugu zangu, msiape kwa mbingu, wala kwa dunia, wala kwa kitu kingine chochote. Semeni “Ndiyo” kama maana yenu ni ndiyo, na “La” kama maana yenu ni la, na hapo hamtahukumiwa na Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Zaidi ya yote, ndugu zangu, msiape, iwe kwa mbingu au kwa dunia, au kwa kitu kingine chochote. “Ndiyo” yenu na iwe ndiyo, na “Hapana” yenu iwe hapana, la sivyo mtahukumiwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini zaidi ya yote, ndugu zangu, msiape, wala kwa mbingu wala kwa nchi; wala kwa kiapo kinginecho chote; bali ndiyo yenu na iwe ndiyo, na siyo yenu iwe siyo, msije mkaangukia hukumu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Juu ya mambo yote kaka zangu na dada zangu, usitumie kiapo unapotoa ahadi, Usiape kwa mbingu wala kwa dunia, ama kwa kitu kingine chochote. “Ndiyo” yenu na iwe “Ndiyo halisi”, na “Hapana” yenu na iwe “Hapana halisi”, ili msije mkaingia katika hukumu ya Mungu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Zaidi ya hayo yote, ndugu zangu, msiape kwa mbingu, wala kwa dunia, wala kwa kitu kingine chochote. Semeni “Ndiyo” kama maana yenu ni ndiyo, na “La” kama maana yenu ni la, na hapo hamtahukumiwa na Mungu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Zaidi ya hayo yote, ndugu zangu, msiape kwa mbingu, wala kwa dunia, wala kwa kitu kingine chochote. Semeni “Ndiyo” kama maana yenu ni ndiyo, na “La” kama maana yenu ni la, na hapo hamtahukumiwa na Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Zaidi ya yote, ndugu zangu, msiape, ama kwa mbingu, au kwa dunia au kwa kitu kingine cho chote. “Ndiyo” yenu na iwe ndiyo, na “Hapana” yenu iwe hapana, la sivyo mtahukumiwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Zaidi ya yote, ndugu zangu, msiape, iwe kwa mbingu au kwa dunia, au kwa kitu kingine chochote. “Ndiyo” yenu na iwe ndiyo, na “Hapana” yenu iwe hapana, la sivyo mtahukumiwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini zaidi ya yote, ndugu zangu, msiape, wala kwa mbingu wala kwa nchi; wala kwa kiapo kinginecho chote; bali “ndiyo” yenu na iwe ndiyo, na “Hapana” yenu iwe hapana, msije mkaanguka katika hukumu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Zaidi ya hayo yote, ndugu zangu, msiape kwa mbingu, wala kwa dunia, wala kwa kitu kingine chochote. Semeni “Ndiyo” kama maana yenu ni ndiyo, na “La” kama maana yenu ni la, na hapo hamtahukumiwa na Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndugu zangu, nilitakalo sana, ni hili la kwamba: Msiape! Msiape na kutaja wala mbingu wala nchi wala kiapo kingine cho chote! Mkisema: Ndio, iwe ndio kweli. Tena mkisema: Sio, iwe sio kweli, kwamba msitumbukie hukumuni!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini zaidi ya yote, ndugu zangu, msiape, wala kwa mbingu wala kwa nchi; wala kwa kiapo kinginecho chote; bali ndiyo yenu na iwe ndiyo, na siyo yenu iwe siyo, msije mkaangukia hukumu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini zaidi ya yote, wandugu zangu, musiape! Musiape kwa jina la mbingu, wala kwa jina la dunia, wala kwa jina la kitu kingine chochote. Museme “Ndiyo” ikiwa munataka kusema ndiyo. Nanyi museme “Hapana” ikiwa munataka kusema hapana, kusudi musihukumiwe na Mungu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini zaidi ya yote, ndugu, msiape kiapo cho chote, kwa mbingu wala kwa inchi; bali ndio yenu iwe ndio, na sio yenu iwe sio, msije mkaangukia hukumu.