James 5:13 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Je, pana mtu yeyote miongoni mwenu aliye na shida? Anapaswa kusali. Je, yuko mwenye furaha? Anapaswa kuimba nyimbo za sifa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Je, mtu yeyote miongoni mwenu amepatwa na taabu? Basi inampasa aombe. Je, kuna yeyote mwenye furaha? Basi na aimbe nyimbo za kusifu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mtu wa kwenu amepatikana na mabaya? Na aombe. Ana moyo wa kuchangamka? Na aimbe zaburi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Je, miongoni mwenu kuna aliye na shida? Anapaswa kuomba. Je, yupo yeyote mwenye furaha? Anapaswa kuimba nyimbo za sifa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Je, pana mtu yeyote miongoni mwenu aliye na shida? Anapaswa kusali. Je, yuko mwenye furaha? Anapaswa kuimba nyimbo za sifa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Je, pana mtu yeyote miongoni mwenu aliye na shida? Anapaswa kusali. Je, yuko mwenye furaha? Anapaswa kuimba nyimbo za sifa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Je, mtu ye yote miongoni mwenu amepatwa na taabu? Basi inampasa aombe. Je, kuna ye yote mwenye furaha? Basi na aimbe nyimbo za kusifu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Je, mtu yeyote miongoni mwenu amepatwa na taabu? Basi inampasa aombe. Je, kuna yeyote mwenye furaha? Basi na aimbe nyimbo za kusifu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kuna mtu miongoni mwenu anayeteseka? Na aombe. Ana moyo wa kuchangamka? Na aimbe zaburi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Je, pana mtu yeyote miongoni mwenu aliye na shida? Anapaswa kusali. Je, yuko mwenye furaha? Anapaswa kuimba nyimbo za sifa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
*Kwenu kama yuko mwenye kuteseka, na amwombe Mungu! Kama yuko mwenye kutulia, na aimbe nyimbo!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mtu wa kwenu amepatikana na mabaya? Na aombe. Ana moyo wa kuchangamka? Na aimbe zaburi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kati yenu kuna mutu anayekuwa katika mateso? Aombe kwa Mungu. Au kuna mutu anayekuwa katika furaha? Aimbe nyimbo za sifa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mtu wa kwenn amepatikana na mabaya? na aombe. Ana moyo wa kuchangamka? na aimbe zaburi.