James 5:15 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakiomba kwa imani mgonjwa ataponyeshwa; Bwana atampatia nafuu, na dhambi alizotenda zitaondolewa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kule kuomba kwa imani kutamwokoa huyo mgonjwa, naye Bwana Isa atamwinua, na kama ametenda dhambi, atasamehewa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa yule, na Bwana atamwinua; hata ikiwa amefanya dhambi, atasamehewa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Maombi yanayofanywa kwa imani yatamfanya mgonjwa apone, na Bwana atampa uzima. Kama atakuwa ametenda dhambi, Bwana atamsamehe.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wakiomba kwa imani mgonjwa ataponyeshwa; Bwana atampatia nafuu, na dhambi alizotenda zitaondolewa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakiomba kwa imani mgonjwa ataponyeshwa; Bwana atampatia nafuu, na dhambi alizotenda zitaondolewa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kule kuomba kwa imani kutamwokoa huyo mgonjwa, naye Bwana atamwinua na kama ametenda dhambi, atasamehewa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kule kuomba kwa imani kutamwokoa huyo mgonjwa, naye Bwana Isa atamwinua, na kama ametenda dhambi, atasamehewa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa yule, na Bwana atamwinua; hata ikiwa amefanya dhambi, atasamehewa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakiomba kwa imani mgonjwa ataponyeshwa; Bwana atampatia nafuu, na dhambi alizotenda zitaondolewa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakimwombea kwa kumtegemea Mungu, vitamwokoa yule mgonjwa, naye Bwana atamwinua tena; kama yuko na makosa, aliyoyafanya, ataondolewa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa yule, na Bwana atamwinua; hata ikiwa amefanya dhambi, atasamehewa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nao wakiomba kwa imani, mugonjwa yule atapona, kwa kuwa Bwana atamurudishia afya yake. Na ikiwa amefanya zambi, atasamehewa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa yule, na Bwana atamwinua; na kama amefanya dhambi, atasamehewa.