James 5:3 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Dhahabu yenu na fedha vimeota kutu, na kutu hiyo itakuwa ushahidi dhidi yenu, nayo itakula miili yenu kama vile moto. Nyinyi mmejirundikia mali katika siku hizi za mwisho!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Dhahabu yenu na fedha yenu zimeliwa na kutu. Kutu yake itashuhudia dhidi yenu, nayo itaila miili yenu kama vile moto. Mmejiwekea hazina kwa ajili ya siku za mwisho.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Dhahabu yenu na fedha yenu zimeingia kutu, na kutu yake itawashuhudia, nayo itakula miili yenu kama moto. Mmejiwekea akiba katika siku za mwisho.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Dhahabu zenu na fedha vimeliwa na kutu! Hiyo kutu itakuwa ni ushuhuda dhidi yenu, na itaila miili yenu kama kwa moto. Mmejilimbikizia mali kwa ajili yenu katika kizazi hiki cha siku za mwisho!
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Dhahabu yenu na fedha vimeota kutu, na kutu hiyo itakuwa ushahidi dhidi yenu, nayo itakula miili yenu kama vile moto. Ninyi mmejilundikia mali katika siku hizi za mwisho!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Dhahabu yenu na fedha vimeota kutu, na kutu hiyo itakuwa ushahidi dhidi yenu, nayo itakula miili yenu kama vile moto. Nyinyi mmejirundikia mali katika siku hizi za mwisho!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Dhahabu yenu na fedha yenu vimeliwa na kutu. Kutu yake itashuhudia dhidi yenu nayo itaila miili yenu kama vile moto. Mmejiwekea hazina kwa ajili ya siku za mwisho.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Dhahabu yenu na fedha yenu vimeliwa na kutu. Kutu yake itashuhudia dhidi yenu nayo itaila miili yenu kama vile moto. Mmejiwekea hazina kwa ajili ya siku za mwisho.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Dhahabu yenu na fedha yenu zimeingia kutu, na kutu yake itawashuhudia, nayo itakula miili yenu kama moto. Mmejiwekea akiba katika siku za mwisho.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Dhahabu yenu na fedha vimeota kutu, na kutu hiyo itakuwa ushahidi dhidi yenu, nayo itakula miili yenu kama vile moto. Nyinyi mmejirundikia mali katika siku hizi za mwisho!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Dhahabu zenu na fedha zenu zimeingiwa na kutu, nazo kutu zao zitawasuta, zitawala nyama za miili yenu kama moto. Mmelimbika mali nyingi siku hizi za mwisho.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Dhahabu yenu na fedha yenu zimeingia kutu, na kutu yake itawashuhudia, nayo itakula miili yenu kama moto. Mmejiwekea akiba katika siku za mwisho.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Zahabu na feza yenu vimepata kutu. Na kutu hii ndiyo itakayowashitaki, nayo itateketeza mwili wenu kama vile moto. Mumejiwekea akiba katika siku hizi za mwisho.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Dhahabu yenu na fedha yenu zimeingia kutu, na kutu yake itakushuhudieni, nayo itakula miili yenu kama moto. Mmejiwekea akiba katika siku hizi za mwisho.