James 5:7 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, ndugu zangu, muwe na subira mpaka Bwana atakapokuja. Tazameni mkulima anavyongoja kwa subira mimea yake itoe mavuno ya thamani. Yeye hungojea kwa subira mvua za masika na za vuli.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo, ndugu zangu, vumilieni hadi kuja kwake Bwana Isa. Tazameni jinsi mkulima angojavyo ardhi itoe mavuno yake yaliyo ya thamani, na jinsi anavyovumilia kwa ajili ya kupata mvua ya kwanza na ya mwisho.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa hiyo ndugu, vumilieni, hata kuja kwake Bwana. Tazama, mkulima hungoja mazao ya nchi yaliyo ya thamani, huvumilia kwa ajili yake hata yatakapopata mvua ya kwanza na ya mwisho.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hivyo kina kaka na kina dada, muwe na subira; hadi kuja kwa mara ya pili kwa Bwana. Kumbukeni kuwa mkulima huyasubiria mazao yake yenye thamani yakue ardhini. Huyangoja kwa subira mpaka yapate mvua za masika na za vuli.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, ndugu zangu, muwe na subira mpaka Bwana atakapokuja. Tazameni mkulima anavyongoja kwa subira mimea yake itoe mavuno mazuri. Yeye hungojea kwa subira mvua za masika na za vuli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, ndugu zangu, muwe na subira mpaka Bwana atakapokuja. Tazameni mkulima anavyongoja kwa subira mimea yake itoe mavuno ya thamani. Yeye hungojea kwa subira mvua za masika na za vuli.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo, ndugu zangu, vumilieni hadi kuja kwake Bwana. Angalieni jinsi mkulima angojavyo ardhi itoe mavuno yake yaliyo ya thamani na jinsi anavyovumilia kwa ajili ya kupata mvua za kwanza na za mwisho.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo, ndugu zangu, vumilieni hadi kuja kwake Bwana Isa. Angalieni jinsi mkulima angojavyo ardhi itoe mavuno yake yaliyo ya thamani na jinsi anavyovumilia kwa ajili ya kupata mvua za kwanza na za mwisho.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa hiyo ndugu, vumilieni, hata kuja kwake Bwana. Tazama, mkulima hungoja mazao ya nchi yaliyo ya thamani, huvumilia kwa ajili yake hata yatakapopata mvua ya kwanza na ya mwisho.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, ndugu zangu, muwe na subira mpaka Bwana atakapokuja. Tazameni mkulima anavyongoja kwa subira mimea yake itoe mavuno ya thamani. Yeye hungojea kwa subira mvua za masika na za vuli.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndugu, vumilieni, mpaka Bwana atakaporudi! Tazameni, mkulima anavyoyangoja mazao ya nchi, maana ni yenye kima! Huvumilia mpaka apate mvua ya vuli nayo ya masika.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa hiyo ndugu, vumilieni, hata kuja kwake Bwana. Tazama, mkulima hungoja mazao ya nchi yaliyo ya thamani, huvumilia kwa ajili yake hata yatakapopata mvua ya kwanza na ya mwisho.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi wandugu, muvumilie mpaka Bwana atakaporudia. Muangalie namna mulimaji anavyongojea shamba litoe mavuno yanayokuwa ya faida kubwa. Yeye anavumilia mpaka wakati mvua ya kwanza na ya mwisho zinaponyesha.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi vumilieni, ndugu, hatta kuja kwake Bwana. Mwangalieni mkulima; hungoja mazao ya inchi yaliyo ya thamani, husubiri kwa ajili yake hatta yatakapopata mvua ya kwanza na ya mwisho.