Jeremiah 1:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Neno la Mwenyezi-Mungu likanijia mara ya pili: “Unaona nini?” Nami nikasema, “Ninaona chungu kinatokota kimeinama upande wangu kutoka kaskazini.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Neno la Mwenyezi Mungu likanijia tena, “Unaona nini?” Nikajibu, “Naona chungu kinachochemka, kikiwa kimeinama kutoka kaskazini.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Neno la Bwana likanijia mara ya pili, kusema, Waona nini? Nikasema, Naona sufuria lenye maji yatokotayo, na mdomo wake unaelekea toka upande wa kaskazini.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Neno la Mwenyezi-Mungu likanijia mara ya pili: “Unaona nini?” Nami nikasema, “Ninaona chungu kinatokota kimeinama upande wangu kutoka kaskazini.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Neno la BWANA likanijia tena, “Unaona nini?” Nikajibu, “Naona chungu kinachochemka kikiwa kimeinama mdomo wake kuelekea upande wa kaskazini.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Neno la bwana likanijia tena, “Unaona nini?” Nikajibu, “Naona chungu kinachochemka, kikiwa kimeinama kutoka kaskazini.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Neno la BWANA likanijia mara ya pili, kusema, Waona nini? Nikasema, Naona sufuria lenye maji yatokotayo, na mdomo wake unaelekea toka upande wa kaskazini.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Neno la Mwenyezi-Mungu likanijia mara ya pili: “Unaona nini?” Nami nikasema, “Ninaona chungu kinatokota kimeinama upande wangu kutoka kaskazini.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Neno la Bwana likanijia mara ya pili kwamba: Wewe unaona nini? Nikasema: Mimi ninaona chungu chenye maji yanayochemka, nao upande wake wa mbele ulioelekea kaskazini umegeuka.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Neno la BWANA likanijia mara ya pili, kusema, Waona nini? Nikasema, Naona sufuria lenye maji yatokotayo, na mdomo wake unaelekea toka upande wa kaskazini.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Neno la Yawe lilinifikia mara ya pili kusema hivi: Unaona nini? Nami nikasema: Ninaona chungu kinachotokota, nacho kinainamia upande wangu tokea kaskazini.