Jeremiah 1:15 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana naziita falme zote za kaskazini na makabila yote. Wafalme wake wote watakuja na kila mmoja wao ataweka kiti chake cha enzi mbele ya malango ya Yerusalemu na kandokando ya kuta zake zote, na kuizunguka miji yote ya Yuda.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nitawaita watu wote wa falme za kaskazini,” asema Mwenyezi Mungu. “Wafalme wao watakuja na kuweka viti vyao vya utawala katika maingilio ya malango ya Yerusalemu, watakuja dhidi ya kuta zake zote zinazouzunguka, na dhidi ya miji yote ya Yuda.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa kuwa, tazama, nitaziita jamaa zote za falme za kaskazini, asema Bwana; nao watakuja, na kuweka kila mtu kiti chake cha enzi mbele ya mahali pa kuingilia malango ya Yerusalemu, na kuzielekea kuta zake pande zote, na kuielekea miji yote ya Yuda.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana naziita falme zote za kaskazini na makabila yote. Wafalme wake wote watakuja na kila mmoja wao ataweka kiti chake cha enzi mbele ya malango ya Yerusalemu na kandokando ya kuta zake zote, na kuizunguka miji yote ya Yuda.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nitawaita watu wote wa falme za kaskazini,” asema BWANA. “Wafalme wao watakuja na kuweka viti vyao vya enzi katika maingilio ya malango ya Yerusalemu, watakuja dhidi ya kuta zake zote zinazouzunguka na dhidi ya miji yote ya Yuda.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nitawaita watu wote wa falme za kaskazini,” asema bwana. “Wafalme wao watakuja na kuweka viti vyao vya enzi katika maingilio ya malango ya Yerusalemu, watakuja dhidi ya kuta zake zote zinazouzunguka, na dhidi ya miji yote ya Yuda.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa kuwa, tazama, nitaziita jamaa zote za falme za kaskazini, asema BWANA; nao watakuja, na kuweka kila mtu kiti chake cha enzi mbele ya mahali pa kuingilia malango ya Yerusalemu, na kuzielekea kuta zake pande zote, na kuielekea miji yote ya Yuda.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana naziita falme zote za kaskazini na makabila yote. Wafalme wake wote watakuja na kila mmoja wao ataweka kiti chake cha enzi mbele ya malango ya Yerusalemu na kandokando ya kuta zake zote, na kuizunguka miji yote ya Yuda.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani ndivyo, asemavyo Bwana: Nitazameni! Ninaiita milango yote ya kifalme wakaao upande wa kaskazini. Nao watakuja, waweke kila mmoja wao kiti chake cha kifalme malangoni mwa Yerusalemu na ng'ambo za kuta zote za boma lake liuzungukalo, hata kwenye miji yote ya Yuda.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa kuwa, tazama, nitaziita jamaa zote za falme za kaskazini, asema BWANA; nao watakuja, na kuweka kila mtu kiti chake cha enzi mbele ya mahali pa kuingilia malango ya Yerusalemu, na kuzielekea kuta zake pande zote, na kuielekea miji yote ya Yuda.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Maana ninaziita falme zote na makabila yote ya kaskazini. Wafalme wake wote watakuja na kila mumoja wao ataweka kiti chake cha kifalme mbele ya milango ya ukuta wa Yerusalema na kandokando ya kuta zake zote, na kuizunguka miji yote ya Yuda.