Jeremiah 1:16 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nami nitawahukumu Waisraeli kwa ajili ya uovu wao wote wa kuniacha mimi, wakafukizia ubani miungu mingine na kuabudu sanamu walizojitengenezea wenyewe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nitatoa hukumu zangu kwa watu wangu kwa sababu ya uovu wao wa kuniacha mimi, kwa kufukiza uvumba kwa miungu mingine na kuabudu kazi za mikono yao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nami nitatamka hukumu zangu juu yao kwa habari ya uovu wao wote; kwa kuwa wameniacha mimi, wakaifukizia uvumba miungu mingine, wakaziabudu kazi za mikono yao wenyewe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nami nitawahukumu Waisraeli kwa ajili ya uovu wao wote wa kuniacha mimi, wakafukizia ubani miungu mingine na kuabudu sanamu walizojitengenezea wenyewe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nitatoa hukumu zangu kwa watu wangu kwa sababu ya uovu wao wa kuniacha mimi, kwa kufukiza uvumba kwa miungu mingine na kuabudu kile ambacho mikono yao imekitengeneza.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nitatoa hukumu zangu kwa watu wangu kwa sababu ya uovu wao wa kuniacha mimi, kwa kufukiza uvumba kwa miungu mingine na kuabudu kile ambacho mikono yao imekitengeneza.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nami nitatamka hukumu zangu juu yao kutokana na uovu wao wote; kwa kuwa wameniacha mimi, wakaifukizia uvumba miungu mingine, wakaziabudu kazi za mikono yao wenyewe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nami nitawahukumu Waisraeli kwa ajili ya uovu wao wote wa kuniacha mimi, wakafukizia ubani miungu mingine na kuabudu sanamu walizojitengenezea wenyewe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, nitakapowatokezea mapatilizo yangu kwa ajili ya ubaya wao wote, kwa kuwa wameniacha wakavukizia miungu mingine, wakatambikia yaliyofanywa na mikono yao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nami nitatamka hukumu zangu juu yao kwa habari ya uovu wao wote; kwa kuwa wameniacha mimi, wakaifukizia uvumba miungu mingine, wakaziabudu kazi za mikono yao wenyewe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nami nitawahukumu Waisraeli kwa ajili ya uovu wao wote, kwa maana waliniacha mimi na kuifukizia miungu mingine ubani na kuabudu sanamu walizojitengenezea wenyewe.