Jeremiah 1:18 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Leo hii nakufanya kuwa imara kama mji uliozungukwa na ngome, kama mnara wa chuma na kama ukuta wa shaba nyeusi, dhidi ya nchi yote, dhidi ya wafalme wa Yuda, wakuu wake, makuhani wake na watu wake wote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Leo nimekufanya mji wenye ngome, nguzo ya chuma, na ukuta wa shaba ili kusimama dhidi ya nchi yote: dhidi ya wafalme wa Yuda, maafisa wake, makuhani wake na watu wa nchi hiyo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana, tazama, nimekufanya leo kuwa mji wenye boma, na nguzo ya chuma, na kuta za shaba, juu ya nchi yote; juu ya wafalme wa Yuda, na juu ya wakuu wake, na juu ya makuhani wake, na juu ya watu wa nchi hii.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Leo hii nakufanya kuwa imara kama mji uliozungukwa na ngome, kama mnara wa chuma na kama ukuta wa shaba nyeusi, dhidi ya nchi yote, dhidi ya wafalme wa Yuda, wakuu wake, makuhani wake na watu wake wote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Leo nimekufanya mji wenye ngome, nguzo ya chuma na ukuta wa shaba ili kusimama dhidi ya nchi yote: dhidi ya wafalme wa Yuda, maafisa wake, makuhani wake na watu wa nchi hiyo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Leo nimekufanya mji wenye ngome, nguzo ya chuma, na ukuta wa shaba ili kusimama dhidi ya nchi yote: dhidi ya wafalme wa Yuda, maafisa wake, makuhani wake na watu wa nchi hiyo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana, tazama, nimekufanya leo kuwa mji wenye boma, na nguzo ya chuma, na kuta za shaba, juu ya nchi yote; juu ya wafalme wa Yuda, na juu ya wakuu wake, na juu ya makuhani wake, na juu ya watu wa nchi hii.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Leo hii nakufanya kuwa imara kama mji uliozungukwa na ngome, kama mnara wa chuma na kama ukuta wa shaba nyeusi, dhidi ya nchi yote, dhidi ya wafalme wa Yuda, wakuu wake, makuhani wake na watu wake wote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tazama! Mimi nimekuweka leo kuwa ngome ya mji na nguzo ya chuma na boma la shaba, nchi zote zishindwe nao wafalme wa Yuda, nao wakuu wao, nao watambikaji wao, nao watu waliomo katika nchi hii.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana, tazama, nimekufanya leo kuwa mji wenye boma, na nguzo ya chuma, na kuta za shaba, juu ya nchi yote; juu ya wafalme wa Yuda, na juu ya wakuu wake, na juu ya makuhani wake, na juu ya watu wa nchi hii.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na tangu leo, ninakufanya kuwa imara kama muji unaozungukwa na kuta, kama munara wa chuma na kama ukuta mugumu sana wa shaba. Utakuwa na nguvu juu ya inchi yote, juu ya wafalme wa Yuda, wakubwa wake, makuhani wake na watu wake wote.