Jeremiah 1:2 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Neno la Mwenyezi-Mungu lilimjia Yeremia mnamo mwaka wa kumi na tatu wa utawala wa Yosia mwana wa Amoni, mfalme wa Yuda.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Neno la Mwenyezi Mungu lilimjia katika mwaka wa kumi na tatu wa utawala wa Yosia mwana wa Amoni mfalme wa Yuda,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ambaye neno la Bwana lilimjia katika siku za Yosia, mwana wa Amoni, mfalme wa Yuda, katika mwaka wa kumi na tatu wa kumiliki kwake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Neno la Mwenyezi-Mungu lilimjia Yeremia mnamo mwaka wa kumi na tatu wa utawala wa Yosia mwana wa Amoni, mfalme wa Yuda.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Neno la BWANA lilimjia katika mwaka wa kumi na tatu wa utawala wa Yosia mwana wa Amoni mfalme wa Yuda,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Neno la bwana lilimjia katika mwaka wa kumi na tatu wa utawala wa Yosia mwana wa Amoni mfalme wa Yuda,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
ambaye neno la BWANA lilimjia katika siku za Yosia, mwana wa Amoni, mfalme wa Yuda, katika mwaka wa kumi na tatu wa kutawala kwake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Neno la Mwenyezi-Mungu lilimjia Yeremia mnamo mwaka wa kumi na tatu wa utawala wa Yosia mwana wa Amoni, mfalme wa Yuda.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Neno la Bwana likamjia siku za Yosia, mfalme wa Yuda, mwana wa Amoni, katika mwaka wa kumi na tatu wa ufalme wake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ambaye neno la BWANA lilimjia katika siku za Yosia, mwana wa Amoni, mfalme wa Yuda, katika mwaka wa kumi na tatu wa kumiliki kwake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Neno la Yawe lilimufikia Yeremia katika mwaka wa kumi na tatu wa utawala wa Yosia mwana wa Amoni, mufalme wa Yuda.