Jeremiah 1:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lilimjia tena wakati Yehoyakimu mwana wa Yosia, alipokuwa mfalme wa Yuda. Yeremia aliendelea kupata neno la Mwenyezi-Mungu hadi mwishoni mwa mwaka wa kumi na moja wa utawala wa Sedekia mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda. Mnamo mwezi wa tano wa mwaka huo, watu wa Yerusalemu walipelekwa uhamishoni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
na pia wakati wa utawala wa Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda, hadi mwezi wa tano wa mwaka wa kumi na moja wa utawala wa Sedekia mwana wa Yosia mfalme wa Yuda, wakati watu wa Yerusalemu walipopelekwa uhamishoni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena lilikuja siku za Yehoyakimu, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda, hata mwisho wa mwaka wa kumi na mmoja wa Sedekia, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda; hata wakati ulipochukuliwa mateka Yerusalemu, katika mwezi wa tano.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lilimjia tena wakati Yehoyakimu mwana wa Yosia, alipokuwa mfalme wa Yuda. Yeremia aliendelea kupata neno la Mwenyezi-Mungu hadi mwishoni mwa mwaka wa kumi na moja wa utawala wa Sedekia mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda. Mnamo mwezi wa tano wa mwaka huo, watu wa Yerusalemu walipelekwa uhamishoni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
pia wakati wa utawala wa Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda, mpaka mwezi wa tano wa mwaka wa kumi na moja wa kutawala kwake Sedekia mwana wa Yosia mfalme wa Yuda, wakati watu wa Yerusalemu walipopelekwa kwenda uhamishoni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
na pia wakati wa utawala wa Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda, mpaka mwezi wa tano wa mwaka wa kumi na moja wa utawala wa Sedekia mwana wa Yosia mfalme wa Yuda, wakati watu wa Yerusalemu walipopelekwa uhamishoni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena lilikuja siku za Yehoyakimu, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda, hadi mwisho wa mwaka wa kumi na mmoja wa Sedekia, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda; hata wakati ulipochukuliwa mateka Yerusalemu, katika mwezi wa tano.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lilimjia tena wakati Yehoyakimu mwana wa Yosia, alipokuwa mfalme wa Yuda. Yeremia aliendelea kupata neno la Mwenyezi-Mungu hadi mwishoni mwa mwaka wa kumi na moja wa utawala wa Sedekia mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda. Mnamo mwezi wa tano wa mwaka huo, watu wa Yerusalemu walipelekwa uhamishoni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Likamjia tena siku za Yoyakimu, mfalme wa Yuda, mwana wa Yosia, mpaka mwisho wa mwaka wa kumi na mbili wa Sedekia, mfalme wa Yuda, mwana wa Yosia, kuufikisha mwezi wa tano wa kuhamishwa kwao Wayerusalemu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena lilikuja siku za Yehoyakimu, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda, hata mwisho wa mwaka wa kumi na mmoja wa Sedekia, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda; hata wakati ulipochukuliwa mateka Yerusalemu, katika mwezi wa tano.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tena lilimufikia Yeremia wakati Yoyakimu mwana wa Yosia, alipokuwa mufalme wa Yuda. Neno la Yawe liliendelea kumufikia mpaka mwisho wa mwaka wa kumi na mumoja wa utawala wa Zedekia, mwana wa Yosia, mufalme wa Yuda. Ni katika mwezi wa tano wa mwaka huo, ndio wakati watu wa Yerusalema walipelekwa katika uhamisho.