Jeremiah 10:12 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu aliiumba dunia kwa nguvu zake; kwa hekima yake aliuimarisha ulimwengu, kwa akili yake alizitandaza mbingu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini Mungu aliiumba dunia kwa uweza wake, akaweka misingi ya ulimwengu kwa hekima yake, na akazitandaza mbingu kwa ufahamu wake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ameiumba dunia kwa uweza wake, Ameuthibitisha ulimwengu kwa hekima yake, Na kwa ufahamu wake amezitandika mbingu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu aliiumba dunia kwa nguvu zake; kwa hekima yake aliuimarisha ulimwengu, kwa akili yake alizitandaza mbingu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini Mungu aliiumba dunia kwa uweza wake, akaufanya ulimwengu kwa hekima yake na kwa ufahamu wake akazitandaza mbingu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini Mungu aliiumba dunia kwa uweza wake, akaweka misingi ya ulimwengu kwa hekima yake, na akazitandaza mbingu kwa ufahamu wake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ameiumba dunia kwa uweza wake, Ameuthibitisha ulimwengu kwa hekima yake, Na kwa ufahamu wake amezitandika mbingu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu aliiumba dunia kwa nguvu zake; kwa hekima yake aliuimarisha ulimwengu, kwa akili yake alizitandaza mbingu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yeye ndiye aliyeifanya nchi kwa uwezo wake, akausimika ulimwengu kwa werevu wake wa kweli, akazitanda mbingu kwa utambuzi wake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ameiumba dunia kwa uweza wake, Ameuthibitisha ulimwengu kwa hekima yake, Na kwa ufahamu wake amezitandika mbingu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe aliiumba dunia kwa nguvu zake; kwa hekima yake alisimamisha ulimwengu imara, kwa akili yake alizitandika mbingu juu.