Jeremiah 10:14 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Binadamu ni mjinga na mpumbavu; kila mfua dhahabu huaibishwa na vinyago vyake; maana, vinyago hivyo ni uongo mtupu. Havina uhai wowote ndani yao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kila mtu ni mjinga na hana maarifa; kila sonara ameaibishwa na sanamu zake. Vinyago vyake ni vya udanganyifu; havina pumzi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kila mtu amekuwa kama mnyama, hana maarifa; Kila mfua dhahabu amefedheheshwa na sanamu yake ya kuchonga; Maana sanamu yake ya kuyeyuka ni uongo, Wala hamna pumzi ndani yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Binadamu ni mjinga na mpumbavu; kila mfua dhahabu huaibishwa na vinyago vyake; maana, vinyago hivyo ni uongo mtupu. Havina uhai wowote ndani yao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kila mmoja ni mjinga na hana maarifa, kila sonara ameaibishwa na sanamu zake. Vinyago vyake ni madanganyo, wala havina pumzi ndani yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kila mmoja ni mjinga na hana maarifa, kila sonara ameaibishwa na sanamu zake. Vinyago vyake ni vya udanganyifu, havina pumzi ndani yavyo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kila mtu amekuwa kama mnyama, hana maarifa; Kila mfua dhahabu amefedheheshwa na sanamu yake ya kuchonga; Maana sanamu yake ya kuyeyuka ni uongo, Wala hamna pumzi ndani yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Binadamu ni mjinga na mpumbavu; kila mfua dhahabu huaibishwa na vinyago vyake; maana, vinyago hivyo ni uongo mtupu. Havina uhai wowote ndani yao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, kila mtu anapopumbaa tu, asijue yatokako, hata kila mfua dhahabu hupatwa na soni kwa ajili ya kinyago chake, kwani alichokitengeneza ni uwongo tu, hata pumzi haimo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kila mtu amekuwa kama mnyama, hana maarifa; Kila mfua dhahabu amefedheheshwa na sanamu yake ya kuchonga; Maana sanamu yake ya kuyeyuka ni uongo, Wala hamna pumzi ndani yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mwanadamu ni mujinga na mupumbafu; kila mufua zahabu anafezeheshwa na sanamu zake. Sanamu hizo ni uongo mutupu, hazina uzima wowote ndani yao.