Jeremiah 10:16 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini Mungu wa Yakobo si kama vinyago hivyo, maana, yeye ndiye aliyeumba vitu vyote, na Israeli ni taifa lililo mali yake; Mwenyezi-Mungu wa majeshi ndilo jina lake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yeye aliye Fungu la Yakobo sivyo alivyo, kwani ndiye Muumba wa vitu vyote, pamoja na Israeli, kabila la urithi wake: Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni ndilo jina lake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yeye, Fungu la Yakobo, siye kama hawa; Maana ndiye aliyeviumba vitu vyote; Na Israeli ni kabila ya urithi wake; Bwana wa majeshi ndilo jina lake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini Mungu wa Yakobo si kama vinyago hivyo, maana, yeye ndiye aliyeumba vitu vyote, na Israeli ni taifa lililo mali yake; Mwenyezi-Mungu wa majeshi ndilo jina lake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yeye aliye Fungu la Yakobo si kama hivi, kwani ndiye Muumba wa vitu vyote, pamoja na Israeli, kabila la urithi wake: BWANA Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yeye aliye Fungu la Yakobo sivyo alivyo, kwani ndiye Muumba wa vitu vyote, pamoja na Israeli, kabila la urithi wake: bwana Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yeye, Fungu la Yakobo, siye kama hawa; Maana ndiye aliyeviumba vitu vyote; Na Israeli ni kabila la urithi wake; BWANA wa majeshi ndilo jina lake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini Mungu wa Yakobo si kama vinyago hivyo, maana, yeye ndiye aliyeumba vitu vyote, na Israeli ni taifa lililo mali yake; Mwenyezi-Mungu wa majeshi ndilo jina lake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini aliye fungu lake Yakobo hafanani navyo, kwani yeye ndiye aliyeyatengeneza yote, naye Isiraeli ni ukoo uliopata fungu kwake; Bwana Mwenye vikosi ni Jina lake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yeye, Fungu la Yakobo, siye kama hawa; Maana ndiye aliyeviumba vitu vyote; Na Israeli ni kabila ya urithi wake; BWANA wa majeshi ndilo jina lake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Mungu wa Yakobo si kama sanamu hizo, maana, yeye ndiye aliyeumba vitu vyote, na Israeli ni taifa linalokuwa mali yake; Yawe wa majeshi, ndilo jina lake.