Jeremiah 10:18 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Wakati huo nitawatupa nje ya nchi hii, nitawataabisha asibaki mtu yeyote.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa kuwa hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: “Wakati huu, nitawatupa nje kwa nguvu wote wanaoishi katika nchi hii; nitawataabisha ili wapate kutekwa.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana Bwana asema hivi, Tazama, wakati huu nitawatupa wenyeji wa nchi hii kama kwa kombeo, nitawataabisha, wapate kuona taabu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Wakati huo nitawatupa nje ya nchi hii, nitawataabisha asibaki mtu yeyote.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa kuwa hili ndilo asemalo BWANA: “Wakati huu, nitawatupa nje kwa nguvu wote waishio katika nchi hii; nitawataabisha ili waweze kutekwa.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa kuwa hili ndilo asemalo bwana: “Wakati huu, nitawatupa nje kwa nguvu wote waishio katika nchi hii; nitawataabisha ili waweze kutekwa.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana BWANA asema hivi, Tazama, wakati huu nitawatupa wenyeji wa nchi hii kama kwa kombeo, nitawataabisha, wapate kuona taabu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Wakati huo nitawatupa nje ya nchi hii, nitawataabisha asibaki mtu yeyote.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Mtaniona mara hii, nikiwatupa kwa nguvu wakaao katika nchi hii, nitawasonga, wapate kuona!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana BWANA asema hivi, Tazama, wakati huu nitawatupa wenyeji wa nchi hii kama kwa kombeo, nitawataabisha, wapate kuona taabu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Maana Yawe anasema hivi: Mara hii nitawatupa inje wakaaji wa inchi hii, nitawataabisha hata kusibaki mutu yeyote.