Jeremiah 10:20 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini hema langu limebomolewa, kamba zake zote zimekatika; watoto wangu wameniacha, na kwenda zao, wala hawapo tena; hakuna wa kunisimikia tena hema langu, wala wa kunitundikia mapazia yangu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hema langu limeangamizwa; kamba zake zote zimekatwa. Wana wangu wametekwa na hawapo tena; hakuna hata mmoja aliyebaki wa kusimamisha hema langu wala wa kusimamisha kibanda changu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hema yangu umetekwa nyara, kamba zangu zote zimekatika; watoto wangu wameniacha na kwenda zao, pia hawako. Hapana mtu atakayenitandikia tena hema yangu, na kuyatundika mapazia yangu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini hema langu limebomolewa, kamba zake zote zimekatika; watoto wangu wameniacha, na kwenda zao, wala hawapo tena; hakuna wa kunisimikia tena hema langu, wala wa kunitundikia mapazia yangu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hema langu limeangamizwa; kamba zake zote zimekatwa. Wana wangu wametekwa na hawapo tena; hakuna hata mmoja aliyebaki kulisimika hema langu wala wa kusimamisha kibanda changu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hema langu limeangamizwa; kamba zake zote zimekatwa. Wana wangu wametekwa na hawapo tena; hakuna hata mmoja aliyebaki wa kusimamisha hema langu wala wa kusimamisha kibanda changu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hema yangu imetekwa nyara, kamba zangu zote zimekatika; watoto wangu wameniacha na kwenda zao, pia hawako. Hakuna mtu atakayenitandikia tena hema yangu, na kuyatundika mapazia yangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini hema langu limebomolewa, kamba zake zote zimekatika; watoto wangu wameniacha, na kwenda zao, wala hawapo tena; hakuna wa kunisimikia tena hema langu, wala wa kunitundikia mapazia yangu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hema langu limeharibika, nazo kamba zangu zote zimekatika; watoto wangu wametoka kwangu, hawako; hakuna atakayelipiga hema langu tena na kuziwamba nguo zangu za hema.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hema yangu umetekwa nyara, kamba zangu zote zimekatika; watoto wangu wameniacha na kwenda zao, pia hawako. Hapana mtu atakayenitandikia tena hema yangu, na kuyatundika mapazia yangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini hema yangu imebomolewa, kamba zake zote zimekatika; watoto wangu wameniacha, na kujiendea, wala hawako tena; hakuna wa kunisimikia tena hema yangu, wala wa kunitundikia mapazia yangu.