Jeremiah 10:22 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sikilizeni sauti! Habari zinatufikia. Kuna kishindo kutoka kaskazini. Taifa kutoka kaskazini linakuja, kuifanya miji ya Yuda kuwa jangwa ambamo kutakuwa na mapango ya mbweha!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sikilizeni! Taarifa inakuja: ghasia kubwa kutoka nchi ya kaskazini! Hii itafanya miji ya Yuda ukiwa, na kuwa makao ya mbweha.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Sauti imesikiwa, Tazama, inakuja; mshindo mkuu kutoka nchi ya kaskazini, ili kuifanya miji ya Yuda kuwa ukiwa, makao ya mbweha.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sikilizeni sauti! Habari zinatufikia. Kuna kishindo kutoka kaskazini. Taifa kutoka kaskazini linakuja, kuifanya miji ya Yuda kuwa jangwa ambamo kutakuwa na mapango ya mbweha!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sikilizeni! Taarifa inakuja: ghasia kubwa kutoka nchi ya kaskazini! Hii itafanya miji ya Yuda kuwa ukiwa, makao ya mbweha.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sikilizeni! Taarifa inakuja: ghasia kubwa kutoka nchi ya kaskazini! Hii itafanya miji ya Yuda ukiwa, makao ya mbweha.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Sauti imesikiwa, Tazama, inakuja; mshindo mkuu kutoka nchi ya kaskazini, ili kuifanya miji ya Yuda kuwa ukiwa, makao ya mbweha.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sikilizeni sauti! Habari zinatufikia. Kuna kishindo kutoka kaskazini. Taifa kutoka kaskazini linakuja, kuifanya miji ya Yuda kuwa jangwa ambamo kutakuwa na mapango ya mbweha!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sikilizeni! Sauti zinasikilika zinazokuja, ni uvumi mkubwa sana upande wa kaskazini! Wanataka kuigeuza miji ya Yuda kuwa mapori tu na makao ya mbwa wa mwitu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Sauti imesikiwa, Tazama, inakuja; mshindo mkuu kutoka nchi ya kaskazini, ili kuifanya miji ya Yuda kuwa ukiwa, makao ya mbweha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Musikilize ile fujo! Angalia inakuja. Kunatokea shindo kubwa upande wa kaskazini. Taifa kutoka kaskazini linakuja kuifanya miji ya Yuda kuwa jangwa, wataigeuza mapango ya mbweha!