Jeremiah 10:5 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Vinyago vyao ni kama vinyago vya kutishia ndege katika shamba la matango, havina uwezo wa kuongea; ni lazima vibebwe maana haviwezi kutembea. Msiviogope vinyago hivyo, maana haviwezi kudhuru, wala haviwezi kutenda lolote jema.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sanamu zao ni kama kinyago kilichowekwa katika shamba la matango kutishia ndege, nazo haziwezi kuongea; na kwa kuwa haziwezi kutembea zinabebwa. Usiziogope. Haziwezi kudhuru wala kutenda lolote jema.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mfano wao ni mfano wa mtende, kazi ya cherehani, hawasemi; hawana budi kuchukuliwa, kwa sababu hawawezi kwenda. Usiwaogope; kwa maana hawawezi kutenda uovu, wala hawana uwezo wa kutenda mema.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Vinyago vyao ni kama vinyago vya kutishia ndege katika shamba la matango, havina uwezo wa kuongea; ni lazima vibebwe maana haviwezi kutembea. Msiviogope vinyago hivyo, maana haviwezi kudhuru, wala haviwezi kutenda lolote jema.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sanamu zao ni kama sanamu iliyowekwa shambani kutishia ndege kwenye shamba la matango, nazo haziwezi kuongea; sharti zibebwe kwa sababu haziwezi kutembea. Usiziogope; haziwezi kudhuru wala kutenda lo lote jema.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sanamu zao ni kama sanamu iliyowekwa shambani la matango kutishia ndege nazo haziwezi kuongea; sharti zibebwe sababu haziwezi kutembea. Usiziogope; haziwezi kudhuru, wala kutenda lolote jema.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mfano wao ni mfano wa mtende, kazi ya cherehani, hawasemi; hawana budi kuchukuliwa, kwa sababu hawawezi kwenda. Usiwaogope; kwa maana hawawezi kutenda uovu, wala hawana uwezo wa kutenda mema.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Vinyago vyao ni kama vinyago vya kutishia ndege katika shamba la matango, havina uwezo wa kuongea; ni lazima vibebwe maana haviwezi kutembea. Msiviogope vinyago hivyo, maana haviwezi kudhuru, wala haviwezi kutenda lolote jema.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Huwa kama nguzo tu iliyofunikizwa, hausemi; sharti uchukuliwe, kwani hauendi. Msiiogope! Kwani haifanyi kibaya, wala haina nguvu ya kutupatia mema.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mfano wao ni mfano wa mtende, kazi ya cherehani, hawasemi; hawana budi kuchukuliwa, kwa sababu hawawezi kwenda. Usiwaogope; kwa maana hawawezi kutenda uovu, wala hawana uwezo wa kutenda mema.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sanamu zao ni kama sanamu za kutishia ndege katika shamba la maboga, hazina uwezo wa kuongea; ni lazima zibebwe maana haziwezi kutembea. Musiziogope sanamu hizo, maana haziwezi kuzuru, wala haziwezi kutenda jambo lolote jema.